Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amefanya mkutano na wananchi Old Kiomboi na Tutu wilayani Iramba.
Mhe: Luhahula amewapongeza walimu na wananchi wa wilaya ya Iramba kwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la Saba wilayani Iramba mwaka huu.” Nawapongeza sana walimu wa wilaya ya Iramba na wazazi kwa kupeleka chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu na hatimaye kupanda kwa ufaulu wa mitihani ya Darasa la saba mwaka huu” Alisema Mhe Luhahula.
Ameongeza kusema wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakiksiha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha watoto masomo “wazazi lazima kuwalinda watoto wao na Wakina mama waache tabia ya kufika wanaume wanaowapa wanafunzi mimba”.
Aidha Mhe Luhahula amesisitiza wananchi kuandaa mashamba kwa wakati kwa kuhakikisha wanaunguza majani yote ili kuua wadudu walioshambulia mahindi mwaka jana.
Vile vile Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa wale ambao wanawaomba Rushwa. “Suala la Rushwa halina mjadala, Rushwa ni adui wa haki, usikubali kununua haki yako, wananchi mnaombwa Rushwa lakini hamtoi taarifa, wananchi toa taarifa ili tuwakamate hao waarifu” alisema Mhe Luhahula.
Kaya nyingi hazina vyoo bora na hali hii itasababisha magonjwa ya kipindupindu. Amewataka wananchi kujenga vyoo bora na ameomba viongozi wa ngazi za vijiji na kata kutoa Elimu kuhusu usafi binafsi, mazingira na kushiriki katika uzoaji takata za majumbani. “Mvua zinaanza kunyesha na vyoo vitaaza kutitia na kuanguka na kuhatarisha maisha yenu, naagiza kila kaya ijenge choo bora na atakayekaidi atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, Wale ambao hawajakamilisha kujenga vyoo wahakikishe vinajengwa na kukamilika na watakao kahidi nitawakama, wananchi hawawezi kufa kwa magonjwa yanayotokana na uchafu, operesheni itaanzishwa kwa ajili ya kubaini kaya zote ambazo hazina vyoo bora na kuchukuliwa hatua kali za kisheria” alisema Mhe. Luhahula.
Mhe: Luhahula amewataka wananchi wa wilaya ya Iramba kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa wahamiaji haramu ili kuthibiti raia wa kigeni na yeyote atayebainika kuficha wahamiaji haramu kwenye eneo lake atachukuliwa hatua kali za kisheria. Alitoa wito kwa wananchi kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka watoe taarifa kwenye vyombo vya daola pale wanapogudua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.