Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amefanya ziara katika kijiji cha Kisonga, Lunsanga kata ya Mtekente pamoja na kijiji cha Luzirukuru tarafa ya Ndago wilayani Iramba ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kufanya mikutano na wananchi ili kuhamasisha shughuli za maendeleo na kusikiliza kero zao leo Tarehe 25.03.2019.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Iramba amekabidhiwa madawati 20 kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisonga kata ya Mtekente tarafa ya Ndago kwa ajili ya shule ya msingi Kisonga ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisonga, Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewashukuru sana kwa ushirikiano wao na kwa kujitoa kuchangia madawati.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Kennedy Thobias Mpanduji, amekabidhi madawati hayo kwa mkuu wa shule ya Kisonga na uongozi wa shule na kuwataka wayasimamie. Aidha amewataka wanafunzi wayatumie vizuri ili baada ya miaka ijayo wadogo zao watakapo kuja wasipate tabu ya madawati na uongozi usichangie tena madawati isipokua wachangie vitu vingine vya maendeleo.
Mhe: Luhahula amewapongeza walimu na wananchi wa kata ya Mtekente kwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa darasa la Saba wilayani Iramba mwaka huu.” Nawapongeza sana walimu wa wilaya ya Iramba na wazazi kwa kupeleka chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu na hatimaye kupanda kwa ufaulu wa mitihani ya darasa la saba mwaka huu. Hongereni sana kwa ushindi wa darasa la saba, watoto wote walifauru kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya msingi Kisonga. wananchi lazima mshirikiane na watalaamu ili kudumisha ufaulu wa wanafunzi wetu. Viongozi wote kuanzia ngazi ya tarafa lazima kuwashirikisha wazazi na kuwaelemisha maana halisi ya Elimu bila malipo na kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule na wanakula chakula. Simamieni suala la utoro na hakikisheni watoto wote wanakwenda shule, hakikisheni watoto wote wanakula chakula shuleni, watoto lazima wale sio ombi kwenye vijiji vyote, ninatumia mamlaka kuagiza hili na sio ombi watoto lazima wale”. Alisema Mhe: Luhahula.
Ameongeza kusema wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakiksiha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha watoto masomo “wazazi lazima kuwalinda watoto wenu na Wakina mama waache tabia ya kufika wanaume wanaowapa wanafunzi mimba”. Ikibainika mtoto wako amepewa mimba, wazazi mtawajibishwa kwa mjibu wa sheria” Alisema Mhe: Luhahula
Aidha Mkuu wa Wilaya Iramba amewataka wananchi kuhakikisha wanasajili watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano ili wapate vyeti vya kuzaliwa ambavyo vimetolewa bure na Mhe: Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt: John Joseph Pombe Magufuli, “mpaka sasa tumekwisha sajili zaidi ya watoto 11,000. Simamieni upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa na hakikisheni mnakitunza maana ukipoteza utalazimika kutoa gharama kukipata ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mhe: Luhahula aliongeza kusema “sote tunaona hali ya hewa, yote tunamwachia mungu lakini hakikisheni wananchi mnatunza chakula, mwenye mfugo avune na kununua chakula maana ni fedhea sana familia kukosa chakula.
Mkuu wa wilaya ya Iramba ameagiza “viongozi kuanzia ngazi ya tarafa simamieni ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo wadogo ili viishe, kufanya hivyo tutakua tunaunga mkono juhudi za Mhe: Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, wajasiliamali wasisumbuliwe, wasitozwe ushuru wowote, wachangie elfu 20,000/= amabyo ni gharama ya kutengeneza kitambulisho hicho, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji simamieni suala hili la vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, Tusimamieni nidhamu, kuheshimiana viongozi wote wa serikali na hakikisheni mnatekeleza wajibu wenu kwa kufanya kazi”. alisisitiza Mhe: Luhahula
Mkuu wa wilaya ya Iramba amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuchangia mapato ili kuleta maendeleo kwenye maeneo yao. “Wananchi tujengee utamaduni wa kutoa mapato. hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemee misaada. Tunahitaji kukamilisha ujenzi wa zahanati ili huduma za afya zipatikane kwa wananchi. jipangeni kuhakikisha majengo haya yanakamalika”. alisema Mhe: Luhahula
Akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo, Mkuu wa wilaya ya Iramba ametembelea ujenzi wa jengo la zahanati ya Mtekente ili kutazama maendeleo ya jengo hilo ambalo limefikia hatua ya lenta.
Vile vile Mhe: Luhahula amewataka Viongozi ngazi ya Tarafa, kata na kijiji kutatua migogoro ya wananchi, kupitia vyombo vya kisheria. Ameongeza kwa kusema “kumetokea wimbi kubwa la mauaji na vifo katika maeneo yenu. Mauaji na vifo hivi vinatokea kwa watu kuuana, kujinyonga, watu kupotea kusipojulikana na watoto kutumbukia kwenye madimbwi/Visima vya maji, “mnafanya unyama, wananchi mnawajua wanaofanya unyama huu, haiwezekani, wazee wangu mnawajua wanaofanya haya sio watu wazima kama nyinyi lakini ni watoto wenu, haiwezekani tukageuza Kisonga kuwa jehanamu, Mwenyekiti wa kijiji, Mtendaji wa kijiji na Mwenyekiti wa kitongoji ambapo matukio haya yametokea paundwe jeshi la ulinzi mara moja. Sitaki kusikia mauaji yanatokea tena. Viongozi kuanzia ngazi ya kata itisha mkutano na kubaini wote wanaofanya mauaji haya” alisisitiza Mhe: Luhahula
Wananchi wanatakiwa kutatua migogoro yao kupitia Ofisi za kiserikali au kwa kuwatumia viongozi wa kijamii walio katika maeneo yao na kwamba kujinyonga au kumuua mtu ambaye una mgogoro/ugomvi naye haisaidiii kutatua mgogoro huo wala kumaliza ugomvi huo. serikali haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria yeyote atayebainika kujiusisha na mauaji.
Ameagiza viongozi na wananchi kuchukua hatua za taadhari katika visima na mabwawa yaliyo katika maeneo yao ili kuepusha vifo vinavyotokana na watoto kutumbukia kwenye mabwawa/visima hivyo na kuwalinda na kuwachunga watoto wao wasicheze katika maeneo hatarishi. “Mtoto akitumbukia kwenye Bwawa/kisima lazima wazazi wachukuliwe hatua kari za kisheria kwa sababu ya uzembe wa kulinda watoto wao” aliongeza kusema Mhe: Luhahula.
Mhe: Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewataka wananchi kudumisha usafi wa mazingira na kuwataka wazazi kuacha tabia ya kuwalea wanafunzi watoro. “Niliagiza kila kaya na taasisi zote kujenga choo bora na watendaji wote kukomesha suala la utoro shuleni, endapo atakapopatikana mwanafunzi mtoro kamata mzazi wake ili tuzalishe watoto wasomi na hatutaki kuzalisha wajinga,” amesema
Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewataka viongozi wa kata kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi kwa wananchi kuhusu fedha mbalimbali wanazozikusanya ili kuwajengea imani ya kufaham fedha iliyochangwa na namna ilivyotumika.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe: Emmanuel Luhahula, amewaomba viongozi wa mazehebu mbalimbali kusaidia serikali kwa kuwafichua wale wote wanaotumia makanisa au misikiti kufanya maovu na kuiombea Wilaya ya Iramba iwe salama. “Niwaomba viongozi wa dini mtusaidie kuwafichua watu wanaotumia vyombo vya dini kufanya maovu. Nilazima viongozi wa dini tulinde amani yetu na kudumisha kulinda amani ya wilaya yetu”.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa wale ambao wanawaomba Rushwa. “Suala la Rushwa halina mjadala, Rushwa ni adui wa haki, usikubali kununua haki yako, wananchi mnaombwa Rushwa lakini hamtoi taarifa, wananchi toa taarifa ili tuwakamate hao waarifu” alisema Mhe Luhahula.
Afisa TAKUKURU wilaya ya Iramba Ndg. Benjamin Masyaga alisema Rushwa ni tatizo ambalo athari zake zinamgusa kila mwananchi. Tatizo hili linasababisha jamii kukosa imani na Serikali yao, amani baina ya wanajamii, kujenga matabaka ya walionacho na wasiokuwa nacho. Vilevile rushwa imekuwa chanzo cha kudhoofisha huduma zinazotolewa katika jamii. “kila mwananchi sehemu alipo aweze kushiriki kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa bila kuchukua muda mrefu. Kila mwananchi anawajibika kuzuia vitendo vya rushwa na kutoa taarifa hizo ili kuchukuliwa hatua stahili za kisheria dhidi ya wala Rushwa na kutokomeza Rushwa nchini.
Ametoa wito wa kukataa kujihusisha na vitendo vya Rushwa ikiwemo kutoa au kupokea Rushwa na kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya Rushwa katika ofisi za TAKUKURU zilizo wilayani Iramba au kwa kupiga simu ya bure namba 113 au kwa vyombo vingine vya dola na viongozi wanaohusika.
Ameongeza kusema wananchi watoe ushirikiano kwa TAKUKURU na vyombo vingine vya dola na kuwa tayari kutoa ushahidi wa vitendo vya Rushwa kwakuwa mara nyingi TAKUKURU imekuwa ikishindwa kufikia malengo kutokana na wananchi kutotaka kutoa ushirikiano
Afisa uhamiaji wilayani Iramba Ndg. Collins Soka amewataka wananchi wa wilaya ya Iramba kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa wahamiaji haramu ili kuthibiti raia wa kigeni na yeyote atayebainika kuficha wahamiaji haramu kwenye eneo lake atachukuliwa hatua kali za kisheria. Alitoa wito huo kwa wananchi kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka watoe taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogudua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao “Mhamiaji haramu ni raia wa kigeni anayeingia nchini na kuendelea kuishi nchini bila kufuata taratibu na sheria za uhamiaji, au anayeingia nchini kwa mujibu wa sheria za uhamiaji lakini akaendelea kuishi nchini kinyume na sheria, kanuni na taratibu. wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za Uhamiaji, kituo cha Polisi, au serikali za mitaa pindi unapohisi kuwepo wahamiaji haramu mahali popote. Ushiriki wako katika kuwafichua wahamiaji haramu ni muhimu sana katika kuimarisha ulinzi, usalama na maendeleo ya nchi”.
Mhe: Mkuu wa Wilaya amewaomba wenyeviti wa vitongoji wote na mabalozi kusimamia na kuimarisha madaftari ya wageni ili kuahakikisha tunatokomeza uhamiaji haram.
Akiongea na wananchi wa Luzirukuru, amewapongeza kwa juhudi zao za kutunza miti "Nimefurahishwa sana na hali ya hewa ya hapa, nimefanya operesheni ya kuzuia ukataji miti. Leo tukisema tufyeke miti, miti yetu itapotea na maeneo haya tutayakimbia, sehemu zingine mazao yamenyauka kwa sababu ya kukata miti na hawapati mvua ya kutosha, Lazima tuifadhi miti ili tuwe na uoto wa asili. Enedeleni kuifadhi misitu ili tuweze kupata mvua. Mvua tunayoipata hapa Iramba inatokana na misitu iliyopo hapa Lunzirukuru, Winduwindu na maeneo mengine, hiyo ndo inatuletea mvua pamoja na ziwa kitangiri". Alisema Mhe: Luhahula
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.