Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe. Emmanuel Luhahula, amekabidhi pikipiki zipatazo 20 kwa Mafisa Elimu Kata Wilayani hapa, katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki kwa Maafisa Elimu Kata, iliyofanyika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri.
Hafla hiyo iliweza kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani ya Halmashauri huku Maafisa Elimu Kata hao kila mmoja akikabidhiwa pikipiki moja kama sehemu yak itendea kazi katika eneo lake.
Pikipiki hizo zimetolewa na serikali kupitia program ya uwezo wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (LANES), zikigharimu jumla ya Tshs. 59,980,000/= bila vati,
Mhe. Luhahula amewaomba viongozi hao kuwa waadilifu na wa mfano wa kuigwa katika matumizi stahiki ya vyombo hivyo alivyokabidhi, na kuwaasa vyombo hivyo vikapate kuwa chachu ya mafanikio katika utendaji na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya kazi.
Amewataka kuvitumia vyombo hivyo kwa tija na kuhakikisha kwamba wanapata mafanikio ya kuboresha Elimu kwa faida ya Umma na si kujitokeza kwa tuhuma za vyombo hivyo kubadilishwa matumizi na kuanza kutumika katika shughuli binafsi na za kibiashara kama vile bodaboda.
Mhe.Luhahula amewapongeza Maafisa Elimu Kata Wilaya ya Iramba, kwa kasi na hatua ya mafanikio wanayokwenda nayo sasa katika kukuza kiwango cha Elimu kwa ongozeko la ufaulu wa daraja la juu huku akichukulia mfano wa matokeo ya mock yaliyotokana Wilaya ya Iramba kuongoza Kimkoa kwa kuwa na wastani wa daraja ‘A’ Asilimia88%.
“Kasi yenu nimeipenda sana, mmenifurahisha na kuukonga moyo wangu. Ninyi mnaweza kuwa chachu kwa viongozi wenzenu ngazi ya Kata mfano maafisa kilimo na watendaji wa Kata kwa sababu miaka yote tangu tunakua, mwalimu ni jeshi anasifa yake ya pekee ya kusikilizwa na kuheshimiwa na kila mtu.” Alisema.
Amewataka kuchochea kasi hiyo ya mafanikio kwa kudumisha ushirikiano na viongozi wa chini pamoja na walimu wao ilikuhakikisha Wilaya ya Iramba inasonga mbele daima.
Aidha maafisa elimu kata hao waliweza kupewa mkataba utakao saidia ufuatiliaji na usimamizi wa utunzaji wa vifaa hivyo ambavyo lengo na madhumuni yake ni kuondoa changamoto zinazokwamisha zoezi la ufuatiliaji wa taaaluma kwa shule zilizopo mazingira ya mbali na kurahisisha usafiri wa maafisa elimu kata katika kazi zao.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.