Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani singida Mhe. Emmanuel Luhahula amezinduzia kampeni ya furaha yangu ya kupima VVU katika viwanja vya machimbo ya Nkonkilangi tarafa ya Shelui leo Tarehe 21.10.2018. Kauli mbiu ya furaha yangu: PIMA, JITAMBUE, ISHI.
Uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu umeudhuliwa na kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe: Samweli Shila, Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni, waheshimiwa madiwani, viongozi mbali mbali wa wilaya ya Iramba na Wananchi.
Mhe. Luhahula amesema Kampeni ya furaha yangu ina lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza na kupima ili kutambua hali zao za maambukizi ya virusi vya UKIMWI na wanaopatikana na maambukizi ya VVU wote waanze kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI ili kuzuia magonjwa nyemelezi na kupunguza wingi wa virusi vya UKIMWI na kuishi kwa furaha na kuendelea na shughuli za kujenga uchumi hasa kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.
Kampeni hii kitaifa ilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungao wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Tarehe 19.6.2018 jijini Dar es salaam na kimkoa ilizinduliwa rasmi mnamo 21.09.2018 na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na leo hii ninazindua furaha yangu kiwilaya katika viwanja hivi vya Nkonkilangi alisema Mhe. Luhahula.
Mhe. Luhahula amewasihi wananchi kutumia fursa hii kama hamasa ili wote kuweza kupima na kutambua hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na watakaopatikana na maambukizi waanze kutumia dawa katika vituo vya afya vya kutolea huduma ya tiba na matunzo na huduma hizi zinatolewa bila malipo ili kuendelea kuishi kwa furaha.
Aliongeza kusema Lengo la kitaifa ni kufikia 2020 asilimia 90 ya wananchi wawe wametambua hali zao za maambukizi na asilimia 90 ya walioambukizwa VVU wawe wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU na asilimia 90 ya wale wanaotumia dawa wingi wa virusi upungue kiwango cha kutoambukiza wengine.
Sambamba na Uzinduzi huu wa furaha yangu amewasihi wananchi kuepuka tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Aidha amesema Viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa la kuhubiri tabia njema zinazoepusha kuendelea kuwepo kwa maambukizi mapya mfano wa biashara ya ngono kwenye madanguro.
Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Iramba Dkt. Timothy Sumbe akisoma taarifa ya utekelezaji wa kudhibiti na kuzuia maambukizi mapya ya ukimwi ameeleza Wilaya ya Iramba imeendeleza mapambano dhidi ya maambukuzi mapya ya VVU kiwango cha maambukizi katika wilaya ni asilimia 2.8% kipindi cha mwaka 2017 ambapo Jumla ya watu 43877 kati yao 18273 walikuwa wanaume na 25604 wanawake walipimwa VVU na kati yao 1206(wanaume:462 na wanawake:744) waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU. Kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka 2018 jumla ya watu 92,159 (wanaume 49234 na wanawake 42, 925) walipima afya zao kati yao, watu 1182(wanaume:441 na wanawake:741) walikutwa na maambukizi ya VVU sawa na asilimia 1.3%. Jumla ya watu 6329(wanaume:2256, wanawake:4073) wameanzishiwa dawa za kufubaza makali ya VVU tangu mwaka 2005 hadi Septemba 2018 sawa na asilimia 82% ya wateja walitegemewa kutambuliwa.
Dkt. Sumbe aliongeza kusema Katika kuhakikisha wilaya inadhibiti maambukizi mapya ya UKIMWI tumejiwekea mikakati mbalimbali kama ifutavyo.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula (mwenye Tshati Nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kupima VVU katika viwanja vya machimbo ya Nkonkilangi tarafa ya Shelui.
Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye foleni wakisubiri kupima afya zao wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha yangu katika viwanja vya machimbo Nkonkilangi tarafa ya Shelui wilayani Iramba.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kupima VVU katika viwanja vya machimbo ya Nkonkilangi tarafa ya Shelui.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula akipima VVU wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kupima VVU katika viwanja vya machimbo ya Nkonkilangi tarafa ya Shelui.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akipima VVU wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kupima VVU katika viwanja vya machimbo ya Nkonkilangi tarafa ya Shelui.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.