Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Iramba Wakili: Boniface Engelberth Kalikona wamekabidhiwa madawati 300 yenye thamini ya Tshs Milioni 30 kwa ajili ya shule za Sekondari na Misingi ili kupunguza upungifu wa madawati Mashuleni kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo Mgodi wa Sekenke Nkonkilangi Wilaya ya Iramba . Waliochangia madawati ni Sekenke one Gold Mine Wamechangia Madawati 115, Iramba Nkulu Gold Mine Wamechangia Madawati 20, Iramba Kenkang’ombe Gold Mine wamechangia Madawati 135, Mgodi wa Mzizini wamechangia Madawati 10 na Kikundi cha hapa kazi tu Mgodi wa Sekenke Kimechangia Madawati 20.
Mkuu wa Wilayaya Iramba amewashukuru sana kwa ushirikiano na kwa kujitoa kuchangia madawati. Amewaomba kila mmoja kwa nafsi yake awiwe na kuchangia madawati.
Vile vile Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewaomba kuifadhi na kutunza Mazingira yawe mazuri ili kuepukana na Magonjwa ya Milipuko.
Sekenke one Gold Mine Wamechangia Madawati 115,
Iramba Nkulu Gold Mine wamechangia Madawati 20,
Iramba Kenkang’ombe Gold Mine Wamechangia Madawati 135
Kikundi hapa kazi tu Mgodi wa Sekenke wamechangia Madawati 20.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.