NA HEMEDI MUNGA
tehama@irambadc.go.tz
Iramba. MKUU wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amepiga marufuku wananchi kufanya shughuli mbalimbali kando mwa vyanzo vya maji.
Mwemda ameeleza hayo leo Jumatano Okotoba 10, 2021 akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji kata ya Maluga Wilayani ya hapa.
Amemtaka Mhandisi wa Maji, Ezra Mwacha kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na iwe na viwango vinavyofanana na fedha iliyotolewa.
Katika hatua nyingine amezitaka Serikali za Vijiji kuhakikisha vinalinda vyanzo vya maji ambapo Serikali imewekeza fedha nyingi ili huduma hiyo itatuwe changamoto ya kupatikana maji kwa muda mrefu.
“Niwaagize Wenyeviti wa Vijiji vyote ambavyo miradi ya maji inatekelezwa kulinda miradi ambayo Serikali inajenga kwa fedha nyingi na kutouza maeneyo ya vyanzo vya maji.” Ameagiza na kuongeza kuwa
“Hakikisheni mmepanda miti katika vyanzo vyote vya maji ili kulinda vyanzo hivyo kwa masilahi yetu wote.”
Halikadhalika, amemtaka Mhandisi wa Maji, Mafundi Sanifu na Venyeviti wa Vijiji katika maeneo mbalimbali yanayotekeleza miradi hiyo kuijenga kwa kiwango bora ili kutimiza makusudio ya Mhe, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha maji yanapatikana kila eneo na muda wote ili kumtua mama ndoo ya maji.
Akiongea na hadhira iliyopo katika ziara hiyo mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Wananchi Wilayani hapo, SSP. Peter Lusesa amewataka wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanatumia sheria ndogo kulinda vyanzo vya maji hali ambayo itawaepusha na migogoro ya hapa na pale.
Awali akitoa tarifa fupi ya utekelezaji wa miradi ya maji mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya, Meneja wa Maji Wilayani hapo, Mhandisi Ezra Mwacha alisema kuwa kazi zinazoendelea katika maeneo yote ambayo miradi inatekelezwa ni ujenzi wa matenki ya kuhifazia maji mita 12 na yenye ujazo wa lita 50,000, nyumba za kuhifadhia mashine (vyanzo vya maji), uchimbaji wa mitaro na DP nane katika kila mradi.
Aidha amefafanua kuwa miradi mitatu aliyoitembelea Mkuu wa Wilaya inatakribani 1.2 Bilioni na kumuhakikishia kuwa ifikapo Machi 2022 miradi itakuwa imekamilika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Zinziligi Tarafa ya Ndago Wilayani hapa, Anthony Kitalu amemshukuru Rais Samia kwa kuwaletea miradi ya maji ambayo inatatua changamoto ya kupata maji waliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu.
“Mhe Mkuu wa Wilaya ! Wananchi hawa wameipokea miradi hii kwa mikono miwili na kukuomba wewe uwafikishie salamu kwa Rais Samia kwa huruma yake ya kuwaletea maji.” Alisema Kitalu
MWISHO
Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye urefu wa mita 12 na lenye ujazo wa lita 50,000 likijengwa kata ya Maluga wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleimani Mwenda akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo wakisikiliza taarifa ya Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye urefu wa mita 12 na lenye ujazo wa lita 50,000 likijengwa kijiji cha Zinziligi wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.