• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amesikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi hekari 420 kati ya Wananchi na Chama cha Ushirika ambapo kila mmoja alidai kuwa hekari hizo ni zao.

Posted on: December 25th, 2021

Na Hemedi Munga

tehama@irambadc.go.tz

Singida - Iramba. Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amesikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi hekari 420 kati ya Wananchi na Chama cha Ushirika ambapo kila mmoja alidai kuwa hekari hizo ni zao.

Mwenda ametatua mgogoro huo leo Ijamaa Desemba 24, 2021 wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha Ushirika na Wananchi wa kijiji cha Nkyala, Kizonzo na Nselembwe Wilayani hapa.

Tangu mwaka 1995 Chama cha Ushirika waliyaacha mashamba haya mpaka leo hii ni takribani miaka 26 ambapo baadhi ya Wananchi waliyavamia na kuanza kuyatumia.

Akiongelea baadhi ya sheria ya ardhi, amesema kuwa mtu anapotumia ardhi kwa miaka 10 na zaidi na hapakuwa na yoyote wakumbuguzi au kumyanganya basi eneo hilo linakuwa lakwake.

Katika kuhakikisha mgogoro huo unatatuka Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maamuzi ya kuzigawa hizo hekari za ardhi.

“ Ndugu zangu hekari 420 ni nyingi sana, hivyo ninazigawa kuwa hekari 210 zitarudi katika Chama cha Ushirika na hekari 210 zibaki kwa Wananchi hawa.” Amesema Mwenda na kuongeza kuwa

“Nawaomba muwe na imani kuwa haki yenu haitapotea kila mmoja atapata eneo ili muendelee na maisha ya kila siku, hivyo hekari hizi tutazigawa kwa utaratibu mzuri.”

Aidha, amewataka Watendaji wa Vijiji kutokuwa chanzo cha kuibua migogoro ya ardhi kati yao na Wananchi hasa kwa kuuza ardhi ambayo haimilikiwi na Serikali ya kijiji.

“Kimsingi yapo makosa yaliofanyika kwa upande wa Chama cha Ushirika kwa kutoacha utaratibu mzuri wa kuyalinda mashamba yao, halikadhalika kwa upande wa Wananchi ambao wamengia kienyeji kwenye mashamba ya Ushirika.”

Pia amewataka Wananchi hao kuhakikisha maeneo au mashamba yao yanapimwa kwa lengo lakuhakikisha mipaka inatambulika nakutosabaibisha migogoro.

“Ndugu zangu ni lazima sasa muhakikishe mashamba au nyumba zenu zinapimwa, eneo, ardhi, bustani au nyumba inapokuwa imekwishapimwa inaongezeka thamani.” alisema

Kutokuwa na hati miliki zinazotambulika kisheria baada ya miaka kadhaa wataingia katika migogoro tena na Chama cha Ushirika na kama sio Chama cha Ushirika basi itakuwa wao kwa wao au na watoto wao kwa sababu watu wanazaliwa lakini ardhi haiongezeki.

Akiongea mbele ya mkuu huyo wa wilaya, Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Singida, Angela Maganga amesema kuwa kwa sababu Wananchi hao wanawezakuwa washirika katikaChama cha Ushirika basi wakubaliane na maamuzi hayo yatakayotolewa.

“Enyi ndugu zangu tambueni kuwa sisi tunawatazama kwa jicho la pili ambapo nyinyi ni wanufaika wa Chama cha Ushirika, tutakuja tuwape elimu ili mjisajili katika Ushirika na kuendelea kunufaika na mambo yanayopatikana katika Ushirika.” Alisema Maganga

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika (SIFAKU), Yahaya Hamisi amesema kuwa wanahitaji kuliendeleza shamba lao kwa kulima zao la alizeti ambayo ipo katika mpango wa kimkoa.

“Ni vyema mkatambua ndugu zangu  msimu huu tumepata mkopo toka benki ya TIDB kwa ajili ya kulima hekari 200.”

Naye mkazi na mdai wa eneo hilo, Rashidi Mayingule amemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa namna ambavyo ametatua mgogoro huo.

“Kwa kweli tunashukuru sana, leo tumepata ufumbuzi wa mashamba haya, hivyo tutaendelea na shughuli zetu za kilimo kwa sababu tayari mvua zimeanza.” amesema

MWISHO

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI June 05, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • DC MWENDA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA AMALI KITUKUTU

    May 08, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    May 06, 2025
  • DC MWENDA ATOA WITO KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUIMARISHA UFUNDISHAJI KWA MADARASA YA MITIHANI

    May 06, 2025
  • JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WILAYANI IRAMBA LATOA ELIMU YA KINGA DHIDI MAJANGA YA MOTO KWA MADIWANI NA WANANCHI

    May 02, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.