Na Hemedi Munga
tehama@irambadc.go.tz
Singida - Iramba. Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amewataka wananchi kulinda na kuuenzi Muungano wa Tanzania ulioasisiwa na Hayati Mwal. Julius K. Nyerere Rais wakwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibari Mzee Abed Karume Aprili 26, 1964.
Mwenda ametoa wito huo leo Jumanne Aprili 26, 2022 wakati wa maadhimisho ya Muungano wa Tanzania akiongea na Wananchi na Watumushi punde baada ya kupanda miti katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya hiyo mjini hapa.
Alisema kuwa kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika jijini Dodoma ambapo viongozi wamekusanyika kujadili nchi hii ilipotoka, ilipo na iendapo kwa lengo la kuimarisha na kudumisha Muungano wa Tanzania.
Akiongea kuhusu Muungano, Mwenda alisema mara kadhaa wamekuwepo maadui wakitamani Muungano huu kuvunjika.
“Ndugu zangu bado wapo watu ndani ya nchi na nje ya nchi wakitamani Muungano huu uvunjike kwa sababu mara kadhaa hoja zinazolenga kuvunjika Muungano katika vikao vya maamuzi katika nchi yetu zimeibuka.” Alisema
Alieleza kuwa mtetezi mkubwa wa Muungano ambaye ni Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwal. Nyerere alifikishiwa hoja ya kuvunja Muungano mara kwa mara.
Alifafanua kuwa Mwal. Nyerere aliitisha Baraza la Mawaziri kwa lengo la kujadili hoja iliyodaiwa kuwa Mzee Karume hautaki Muungano kipindi hicho.
“Taarifa hizi zilimuumiza sana Mwal. Nyerere na kuita Baraza la Mawaziri kujadili suala la Muungano.” Alisimulia na kuongeza kuwa
Mmoja kati ya wasaidizi wa Mwal. Nyerere alimshawishi Mwal. Nyerere kuwa yupo Katibu Mkuu wa ASP Mzee Thabit Kombo hapa Dar es Salaam ni vyema aitwe ili aulizwe madai haya ya hoja ya kuvunja Muungano.
Baada ya Mzee Thabit Kombo kufika mbele ya Mwal. Nyerere nakuelezwa madai haya, Mzee Kombo alisema kuwa jambo hili sio kweli kwa sababu Mzee Karume hawezi kuja na hoja ya kuvunja Muungano.
“Naomba nikuthibitishie niende nikamuulize Mzee Karume.”
Katika kuhakikisha Mzee Kombo anapata uhakika wa hoja hii, Mzee Kombo na Mmoja wa wasaidizi wa Mwal. Nyerere walikwenda kuonana na Mzee Karume.
Baada ya kukutana na Mzee Karume na kumueleza madai haya, Mzee Karume alisema kuwa hilo jambo halipo ni uongo kabisa na nijambo la kutengeneza na sijui ni nani kamuaminisha Mwal. Nyerere jambo hili.
Hatimaye Mzee Kombo na Mmoja wa wasaidizi wa Mwal. Wakarejesha majimbu kwa Mwal. Nyerere kuwa Mzee Karume alisema kuwa hilo jambo ni uongo na ni ufitini wa hali ya juu.
“Kwa kweli ni uongo, kwa sababu Mzee Karume alisema kuwa hajawahi, kutamka, kunongona, kuandika wala kufikiria juu ya kuvunja muungano huu.” Alimthibitishia Mwal. Nyerere Mzee Kombo
Hali hii ilimfanya Mwal. Nyerere kufurahi na kumkumbatia Mzee Thabit Kombo na kuwaruhurusu mawaziri kurejea nyumbani kwa sababu hakuna tena Baraza la Mawaziri.
“Sasa ni wjibu wetu kuulinda na kuuenzi Muungano wetu kwa sababu watu ambao wanaopinga Muungano bado wapo ndani ya nchi yetu na nje ya nchi ili waone tu Tanzania imevunjika.” Aliomba Mkuu huyo wa wilaya
Aidha, aliongeza kuwa Muungano ni nembo inayobeba uhai wa Taifa na kuchangia uhai wa wanadamu na viumbe vingine kupitia uwepo wa miti na uoto wa asili, hivyo tunapaswa kuendelea kutunza na kulinda uoto wa asili katika mazingira yetu.
Wananchi wa Iramba katika kuhakikisha wanatunza mazingira wameafinikiwa kupanda miti takribani 238 kati ya miche 500 iliyokusudiwa kupandwa.
Kufuatia hali hiyo, Mwenda aliwataka wananchi hao kuendelea kuhamasishana kulinda na kutunza maliasili na miti na kuwa wakali wa waharibifu wa miti na maliasili.
Alisema miaka 58 ya Muungano wa Tanzania kumekuwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa ambayo kwa sehemu kubwa yanatokana na uharibifu wa mazingira.
Aidha, alitolea mfano wa Msitu wa Sekenke Tulya ambao miaka takribani 40 iliyopita kulikwa na wanyama wa kila aina mfano wa nyumbu, nyanti, tembo na faru ambapo kutokana na uharibu wa mazingira wanyama wote wamehama.
Akiongelea kuhusu hali ya hewa miaka ya nyuma Iramba watu walikuwa wakivaa makoti kwa sababu ya baridi lakini sasa haiwezekani.
Pia, alitolea mfano wa nchi ya China katika mji wa Bejin ambapo hufika msimu watu hawavai makoti wala shati kwa kuroa kutokana na nyuzi joto kufikia 42 mpaka 45, hali ambayo ilichangiwa na kutumia makaa yamawe kuendesha viwanda vyao.
“Niwaombe! Tulinde mazingira yetu.”
Akiongea katika hafla hiyo katibu wa jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Iramba, Mwal. Iddi Kijamba aliwataka watanzania kuendelea kuuenzi na kuulinda muungano wa Tanzania kwa gharama yoyote.
Alibainisha kuwa Muungano uliokusudiwa na waasisi wetu ulikuwa ni kuhakikisha uhusiano wa kiudugu, kisiasa, kilugha na kibiashara unatamalaki.
“Muungano huuo ndio unaotufanya sisi watanzania tuishi bila ya kubaguana na kuwa wamoja na kudumisha amani na utulivu.” Alisema Kijamba
Aidha, alisema kuwa tuwakatae kila ambaye ataleta chochoko za kutaka kuvunja muungano, kwa sababu watu hao hawana nafasi katika jamii ya watanzania.
Naye Afisa Mazingira wa wilaya hiyo, Yohana Dondi alimshukuru Mkuu wa wilaya hiyo kwa kufanikisha maadhimisho ya Muungano wa Tanzania kwa kupanda miti kwa namna taratibu na kanuni zinavyoelekeza.
“Kwa kweli tumefanya vizuri kwa sababu wananchi wameadhimisha muungano kwa kufanya usafi na kupanda miti ili kuifanya Iramba ya kijani.”
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.