Hemedi Munga Irambadc
Singida - Iramba. MKUU wa Wilaya ya Iramba,
Suleiman Mwenda amefanikiwa kubadhi fedha za Wakulima wa Pamaba zilizodaiwa kuliwa na viongozi wa Chama cha Msingi cha Ushirika wa Wakulima wa Pamba chenye namba za usajili SIR 3454 Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwenda amekabidhi fedha hizo leo Jumanne
Oktoba 12, 2021 wakati akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Lutamla alipofanya zira kijijini hapo.
Takribani Tsh Milioni kumi (10,000,000) imekwisha kamilika ambayo itakabidhiwa kwa wananchi 178 ambao walikuwa hawajalipwa baada ya kudaiwa kuwa viongozi wa chama hicho kupata hasara.
“Ndugu zangu Wananchi baada ya uchunguzi toka kwa Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Singida, tumefanikwa kurejesha fedha hizo na leo kila mwenye risiti atapatiwa fedha zake na hakuna mwananchi ambaye atakayedhulumiwa.” Amesema Mwenda
Halikadhalika, alibainisha kuwa kwa wale ambao hawana risiti utaratibu wao unaandaliwa na watalipwa fedha zao hivi karibuni.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mwenyekiti wa
Kijiji cha Lutamla Kata ya Mtoa Wilayani hapo, Ngasa Ngasa alisema kuwa chanzo cha kuchelewa kulipa fedha za wakulima wa pamba kijijini hapo kinatokana na viongozi wa chama cha Ushirika huo kununua pamba na kudai kuwa wamepata hasara ya takribani milioni Ishirini na mbili ( 22,000,000).
Ngasa amewataja viongozi hao kuwa ni Shabani Juma Mwenyekiti wa Ushirika, Stephano Msengi katibu wa ushirika na Hamisi Msengi mhasibu wa Ushirika huo.
Kwa sababu Wakulima wa pamba ndio tegemeo la zao la pamba Mkoani Singida walidai kuwa wameibiwa na viongozi hao, jambo ambalo lilimfanya Mkuu wa Wilaya hiyo kuagiza uchunguzi ufanyike na hatimaye leo wakulima hawa wanalipwa fedha zao. Aliongeza Ngasa
Kwa upande wake mmoja wa wakulima wa pamba wa kijiji hicho, Rasa Kasinili alimshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kufanikisha zoezi la kuwagawia fedha zao na kuwaasa wakulima wenzake kuwa wazitumie fedha hizo katika kulima kilimo cha pamba katika msimu huu mpya na siyo kizitumia kunywa pombe na anasa nyinginezo zinazorudisha maendeleo yao nyuma.
“Mpaka sasa Mkuu wa Wilaya amefika hapa akiwa na fedha zetu, tunajisikia faraja kupata fedha hizo na tunampongeza Mkuu wa Wilaya.” Alishukuru Kasinili
Naye Lameck Nyorobi wa kijiji hicho alisema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kutau mgogoro huo ambao ulikuwa unawanyima haki wakulima wapamba.
MWISHO.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akitoa mrejesho wa namna alivyofanikisha kupata fedha za wakulima wa pamba ambao wanaodaiwa kudhulumiwa na Viongozi wa Chama cha Ushirika kijiji cha Lutamla Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akitoa mrejesho wa namna alivyofanikisha kupata fedha za wakulima wa pamba ambao wanaodaiwa kudhulumiwa na Viongozi wa Chama cha Ushirika kijiji cha Lutamla Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Ugawaji fedha za wakulima wa pamba ambao wanaodaiwa kudhulumiwa na Viongozi wa Chama cha Ushirika kijiji cha Lutamla Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Mkoa wa Singida ukiendelea. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.