Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akitatua kero mbalimbali zilizowasilishwa kwake na wananchi wa Kaselya na Ndulungu .
Wananchi wa kata ya Kaselya wakisikila utatuzi wa kero toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda. Picha na Hemedi Munga
Diwani wa kata ya Kaselya, Juma Nakwaula akiwasilisha kero kwa niaba ya wanachi wa kata hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda. Picha na Hemedi Munga
Wananchi wakifuatilia kwa makini utatuzi wa kero toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda. Picha na Sarapion Kakiziba
Diwani wa kata ya Ndulungu, Salumu Bunyongoli akiwasilisha kero kwa niaba ya wananchi kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda. Picha na Sarapion Kakiziba
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amesikiliza na kutatua kero za wananchi zilizowasilishwa na madiwani wa kata ya Kaselya na Ndulungu.
Mwenda ametatua kero hizo leo jumanne Julai 27, 2021 wakati alipofanya ziara katika kata hizo zilizopo Wilayani Iramba Mkoani Singida.
Akiwasilisha kero za wananchi mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya Diwani wa Kata ya Kaselya, Juma Nakwaula amesema kuwa kuna changamoto ya barabara tokea Milade, Sepuka hadi Ussure na kuomba uongozi kukamilisha ujenzi wa Zahanati ili ianze kutoa huduma.
Nakwaula amebainisha changamoto ya kupata hati za kimila ziweze kutambulika ili zisaidie katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Aidha ameomba uongozi kuhakikisha kuwa dawa zinapatika kwa wananchi waliokata kadi za iCHF.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ndulungu, Salumu Bunyongoli amewasilia kero za wananchi mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwa kata hiyo haina shule ya sekondari na uwepo wa changamoto ya barabara iendayo shule ya msingi Kipuma.
Aidha Bunyongoli amefafanua kuwa wananchi wa kata hiyo wanapata tabu ya upatikanaji wa huduma za afya kwa sababu hulazimika kuzifuata kata ya Ndago.
Akitatua kero mbalimbali zilizowasilishwa na Madiwani kwa nyakati tofauti tofauti Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imetenga fedha katika bajeti zake kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari Ndulungu.
Mwenda amewahakikishia wananchi kuwa barabara ya kutoka Kizaga hadi Sepuka ipo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu CCM ni chama sikivu na chenye kukamilisha ilani yake ni wahakikishie kuwa barabara hiyo itaanza ujenzi hivi karibuni na kukamilika kwa viwango bora kwa wakati.
Pia amewataka Watendaji wa Kata Wilayani Iramba kuwatambua Wazee waliopo katika maeneo yao ili waweze kupata matibabu kwa wakati katika Zahanati, vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya.
Aidha ameitaka taasisi ya TANESCO kuhakikisha inafikisha umeme katika shule ya Msingi Mgungia.
Katika hatua nyingine, Mwenda amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kuhakikisha anafanya tathimini ya soko la madini Ndulungu – Kipuma.
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.