Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda ameahidi kutokomeza mimba za Utotoni
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akimkabidhi vitabu vya kiada na ziada Mwalimu wa Shule ya Utayari Kisingu iliopo kata ya Ulemo Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Diwani wa Viti maalumu Wilayani Iramba, Winjuka Songelael ameahidi kutoa gunia 2 za mahindi na sukari kilo 25 kwa lengo la kuhakakikisha wanafunzi wa Utayari Kisingu wanakunywa uji wawapo katika kituo hicho. Picha na Hemedi Munga
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Chacha Kehogo akiipongeza Serikali ya kijiji cha Kitukutu Kisingu Wilayani Iramba kwa kufanikisha kutoa eneo lenye ukubwa wa hekari 21 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kielimu. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akikagua kituo cha Utayari Kisingu kilichojengwa Kata ya Ulemo Wilayani Iramba kwa ushirikiano wa Shirika la SEMA na Serikali. Picha na Hemedi Munga
Furaha ya wanafunzi wa Utayari Kisingu wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda alipotembelea na kukagua jengo la Utayari Kisingu kwa lengo la kukabidhiwa jengo hilo. Picha na Hemedi Munga
Kutuo cha Utayari Kisingu kilichojengwa Kata ya Ulemo Wilayani Iramba kwa ushirikiano wa Shirika la SEMA na Serikali kwa garama ya Tsh 29 milioni. Picha na Hemedi Munga
Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda ameahidi kutokomeza mimba za utotoni kwa wanafunzi na kuendelea kusimamia kwa ukaribu suala la elimu ili kuinua ufaulu wa shule zilizopo Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwenda ametoa ahadi hiyo leo Ijumaa Julai 9, 2021 wakati akiongea na wananchi wa Kitukutu kata ya Ulemo Wilayani Iramba katika hafla ya makabidhiano ya Kituo cha Utayari Kisingu yaliofanyika kijijini hapo.
Amewaomba wazazi kufahamu kuwa wanalojukumu la kuhakikisha malezi ya watoto wao yanakua bora na kuhakikisha wanafunzi wanatimiza ndoto zao.
“Ndugu wananchi! tuwalinde vijana wetu kutokana na tatizo la mimba, hivyo ninakemea Wilaya nzima kuhakikisha hakuna mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi” amesisitiza Mwenda na kuahidi kuwa
“Nimekuja kutokemeza suala la mimba za utotoni, hivyo nimuombe kila aliyopo hapa kuwa mjumbe wakumfikishia taarifa asiyekuepo hapa kuwa mimba za utotoni sasa basi.”
Amewataka kufahamu kuwa yoyote atakayethibishwa kumtia mimba mwanafunzi atahukumiwa kwenda jela miaka thelathini.
Aidha mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi kuchangia mahindi ili kuhakikisha watoto wa shule ya Utayari wanapata uji na kwa wale wa shule za msingi na Sekondari wanapata chakula.
Akisoma risala fupi mbele ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Mradi wa Shirika la SEMA, Mauth Cosmas amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la SEMA wametekeleza mradi huu wa jengo la Elimu ya Awali Malezi na Makuzi kwa hadhi ya kisasa.
Cosmas amebainisha kuwa jamii ilijitolea mchanga na mawe vyenye jumla ya Tsh 2.9 milioni huku Shirika la SEMA wakitoa Tsh 26 milioni kukamilisha kituo cha Utayari chenye hadhi ya kisasa.
Kufuatia uwepo wa kituo hicho cha kisasa kumeongeza idadi ya wanafunzi kuwa 88 ambapo 43 ni wasichana na 45 ni wavulana ikiwa ni sawa na ongezeko la 75% ukilinganisha na idadi iliyokuepo mwaka 2018.
Kukamilika na kutumika kwa jengo hili kumevutia watoto toka vijiji vya pembezoni kuja kusoma hapa, hivyo kuongeza udahili katika shule mama ya Kitukutu ambapo jumla ya wanafunzi 65 wamejiunga na darasa la kwanza mwaka 2021.
Akiongea katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Chacha Kehogo amelipongeza Shirika la SEMA kwa kushirikiana na Serikali kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha Utayari.
Pia amweshukuru wananchi ambao walitoa eneo na kuwaahidi kuwa hapo patajengwa shule kadri uwezo utakavyopatika.
“Nipongeze Serikali ya kijiji iliyotoa eneo hili lenye ukubwa wa hekari 21 na niwaahidi kuwa hapa patakua na shule” ameahidi Kehogo
Naye Meneja wa Sirika la SEMA, Ivo Manyaku amegawa vitambu vya kiada na ziada kwa lengo la kuwezesha ufundishaji na kuinua taaluma kwa wanafunzi hao.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Benard Kisuka ameishukuru Serikali kwa kushirikiana na SEMA kufanikisha ujenzi wa kituo hicho cha Utayari kijijini hapo.
SEMA wamefanikiwa kukikabidhi kituo cha Utayari kilichojengwa kwa jumla ya Tsh 29 milioni kwa Serikali ili iendelee kukilea na kuboresha mazingira yanayozunguka kituo hicho.
Mwisho.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.