Hemedi Munga Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amerudisha rasmi shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa Sekenke one uliokuwa umefungwa tangu mwaka 2019 Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwenda amerudisha uchimbaji wa Madini katika Mgodi huo leo Jumatatu Agasti 02, 2021 wakati akiwa katika ziara zake za utatuzi wa kero mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
“Mimi ni Msimamizi wa usalama wa raia ikiwa nimehakikishiwa kuwa wachimbaji hawa watakwenda ardhini na kurudi wakiwa salama basi sina pingamizi sasa narudisha rasmi shughuli za uchimbaji hapa” ameruhusu Mwenda
Kwa kuzingatia thamani na umuhimu wa wachimbaji wadogo wenye mchango mkubwa nchini, tunaruhusu vijana waje hapa waendelee na shughuli za uchimbaji ambazo zitakuwa zimewapatia ajira na kutimiza mpango wa serikali.
Aidha amewataka wajumbe wa Bodi ya Sekenke one kuhakikisha wanazingatia kanuni na taratibu katika uchimbaji wa duara 00 na 27 na mengine yaliokuwa salama kwa namna ya utafiti uliofanywa na wataalamu.
Pia ameionya Bodi ya Sekenke One kuto yaendea maduara 12 yaliokatazwa kutokana na changamoto anuai katika eneo hilo.
Hatua hii imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Waziri wa Madini, Dotto Biteko alipofanya ziara ya ukaguzi wa soko la madini liliopo Shelui Wilayani hapo Julai 31, 2021.
Akiongea na wataalamu pamoja na wachimbaji wadogo wadogo waliofika katika soko hilo, Biteko aliwaambia kuwa usalama wa nchi upo kwa hawa wachimbaji wadogo wadogo kwa sababu wachimbaji wakumbwa muda wowote wanaweza kuhama au kuondoka.
“Turudishe nguvu kwa wachimbaji wadogo kwa sababu wakifanya kazi kwa weledi huwezi kuona uwazi uliopo kati yao na wachimbaji wakubwa,” alisema Waziri nakuongeza kuwa
“Nikuagize Kaimu Afisa Madini Mkazi kukutana na hawa wachimbaji wadogo wadogo endapo watakuandikia barua ya kujidhamini katika uchimbaji wao dhidi ya eneo hili basi wafunguliwe shughuli za uchimbaji ziendelee.”
Kwa upande wake Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo amemuhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wachimbaji hao walikwisha andika barua ya kujidhamini kuchimba katika maeneo yaliokua salama katika eneo hili.
Malembo alifafanua kuwa maeneo hayo ni duaara namba 00 na 27, huku akiwataka kutofika katika maduara 12 yalikuwa na changamoto anuai.
Naye katibu wa Bodi ya Sekenke one ambaye ni mmoja wa miliki wa Mgodi huo, Joseph Mnemba ameishukuru serikali kwa kufungua mgodi huo kwa sababu maisha ya wananchi yalikua magumu, hivyo wanamuomba Mungu awasadie neema zipatikane ili kila mmoja apate kipato.
Mgodi wa Sekenke one una leseni mbili za mgodi wa Sekenke namba moja na Sekenke namba mbili ambazo zilifungwa mnamo Novemba 9, 2019 kutokana na changamoto anuai. Sasa shughuli za uchimbaji zitaendelea na kurudisha uchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.