Hemedi Munga Irambadc
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amewapongeza viongozi na wananchi wote kwa kufanikisha kuupokea Mwenge wa Uhuru ukiwa unawaka, unameremeta, kufanikiwa kuutunza na kuukimbiza Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwenda ametoa pongezi hizo leo Jumatano Julai 21, 2021 punde baada ya kumkabidhi wakimbiza mbio maalum za Mwenge wa Uhuru kitaifa na Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Mfaume katika viwanja vya kijiji cha Kidii kata ya Msingi Wilayani hapo.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa viongozi na wananchi wa Iramba mnastahili pongezi kwa namna ambavyo mmekua mstari wa mbele tangu maandalizi ya miradi ya maendeleo na shughuli zote zilizotembelewa kuhakikisha zinakamilika kwa wakati na ubora unaohitajika.
Mwenda amebainisha kuwa miradi yote iliotembelewa na Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru zilikua na garama ya takriban Tsh 1.8 bilioni.
Aidha amefafanua kuwa fedha hizo zimechangiwa na nguvukazi (wananchi) kwa kutoa Tsh 7.5 milioni sawa na asilimia 0.4, Serikali kuu imetoa Tsh 517.8 milioni sawa nasilimia 27.5 huku Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ikiwa imetoa Tsh 12 milioni sawa na asilimia 0.6 na Wahisani kutoa Tsh 1.3 bilioni sawa na asilimia 71.4.
Hivyo Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru zimezindua mradi wa barabara ya mchepuo iendayo Hospitali kongwe ya Kiomboi, jengo la Uthibiti ubora wa Elimu liliopo mjini kiomboi na Mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Kyalosangi Tarafa ya Kinampanda Wilayani hapa.
Aidha Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimefanikwa kutembelea na kuona shughuli sita (6).
Awali akifikisha ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa wananchi katika kijiji cha Misigiri kiongozi wa wakimbiza Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Paul amewataka wananchi hao kuwa mabalozi wa kufikisha ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria katika mbio hizo.
Akieleza ujumbe Mkuu wa Mwenge wa Uhuru unaoonesha dira ya Taifa letu uliobeba kauli mbiu isemayo “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; itumie kwa usahihi na Uwajibikaji” amewataka wananchi kuitumia TEHAMA kwa usahihi na kujipatia habari, ajira na kusoma kwa njia ya mtandao nakutolea mfano kuwa unaweza kuwa Iramba huku unasoma chuo kikuu cha Dodoma ( UDOM) au chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Pia kwa kutumia TEHAMA imekua rahisi kununua bili za maji na umeme na kufanikiwa kuondoa adha ya kupanga foleni na kupoteza muda.
“Ndugu Wananchi nitoe wito kwenu kuhakikisha mnadai risiti za kielektroniki pale mtakapo kua mmenunua bidhaa yoyote au kupata huduma yoyote” amesisitiza Luteni Paul na kuongeza kuwa
“Niziagize Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakusanya mapato kielektroniki.”
Aidha amebainisha ujumbe wa kudumu wa mapambano dhidi ya Rushwa yenye kauli mbiu isemayo “Kupambana na Rushwa ni Jukumu langu”, hivyo amewataka wananchi kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya rushwa kwa mamlaka zinazohusika ili nchi isonge mbele.
Katika hatua nyingine Luteni Paul amewataka wananchi kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria chini ya kauli mbiu isemayo “Ziro Malaria inaanza na Mimi-Nachukua hatua kuitokomeza.” Hivyo awataka wananchi kuutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kufukia madibwi na kuhakikisha wanalala ndani ya chandarua.
Pia amewakumbusha wananchi kuendeleza mapmbano dhidi ya madawa ya kulevya chini ya kauli mbiu isemayo “Elimu sahihi juu ya Dawa za kulevya huboresha huduma kwa Waraibu; chukua hatua.”
Amewataka wanacnhi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za watu wanozalisha, safirisha au kuuza dawa za kulevya ili wawezekuchukuliwa hatua, hatimaye kutokomeza kabisa suala la madawa ya kulevya nchini.
Aidha amewahimiza wanachi kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI chini ya kauli mbiu isemayo “Mshikamano wa Kitaifa; Tuwajibike kwa pamoja.” Hivyo ni wajibu wa wazazi kuwapa elimu vijana namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI na kuwa na tabia ya kupima mara kwa mara ili kutambua afya zao.
Halikadhalika amewaasa wazazi kuhakikisha wanatoa lishe bora kwa watoto chini ya kauli mbiu isemayo “Tujenge Jamii yenye Afya Imara kwa kuzingatia lishe bora.”
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Shelui, Ernestina Shuka ameonesha kuwa ujio wa Mwenge wa Uhuru umekua na faida kubwa kwa sababu wamejipatia elimu ya namna ya kujikinga kujingiza katika madawa ya kulevya na hatua za kushauri kwa mtu alieathirika na madawa ya kulevya ili aweze kuacha kabisa matumizi ya madawa ya kulevya.
Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kilometa 163.4 kutoka eneo la kupokelea Malendi na kupita katika tarafa 3, kata 7 na vijiji 12 mpaka sehemu ulipokabidhiwa kijiji cha Kidii kata ya Msingi Wilayani Mkalama Mokani Singida.
MWISHO
Katibu Tawala Wilaya ya Iramba, Pius Songoma akisoma Risala ya Utii kwa Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Kulia ni Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo, B’hango Lyangwa. Picha na Hemedi Munga
Kiongozi wa Wakimbiza mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Paul akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge kwa wananchi walihuohudhuria mbio hizo. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda kushoto akiwa na Kiongozi wa wakimbiza Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru katikati, Luteni Josephine Paul pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru wengine wakikagua barabara ya mchepuo iendayo hospitali kongwe ya Kiomboi tayari kwa kuizindua. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda watatu kutoka kushoto akiwa na Kiongozi wa wakimbiza Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru katikati, Luteni Josephine Paul pamoja na wajumbe wengine wakitroti baada ya kukagua barabara ya mchepuo iendayo hospitali kongwe ya Kiomboi tayari kwa kuizindua. Picha na Hemedi Munga
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Shelui aliyo katika klabu ya kupiga vita madawa ya kulevya, Ernestina Shuka ameonesha kuwa ujio wa Mwenge wa Uhuru umekua na faida kubwa kwa sababu wamejipatia elimu ya namna ya kujikinga kujingiza katika madawa ya kulevya na hatua za kushauri kwa mtu alieathirika na madawa ya kulevya ili aweze kuacha kabisa matumizi ya madawa ya kulevya. Picha na Hemedi Munga
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakisikiliza ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mara ulipowasili katika viwanja vya shule ya msingi shelui . Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.