Na Hemedi Munga
tehama@mgail.go.tz
Singida - Iramba. MKUU wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amewataka Madiwani kuwa wakali dhidi ya wale wanaotorosha mazao.
Mwenda ametoa wito huo juzi wakati wa salamu za viongozi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Kuziba njia zote zinazotumika kutorosha mazao kutaifanya Halmashauri hii iweze kukusanya mapato na kuweza kuingia kumi bora katika ukusanyaji wa mapato ukilinganisha na Wilaya ya Meatu na Igunga zilizo jirani.
“Waheshimiwa Madiwani! wito wangu kwenu tuhakikishe tunasimamia Halmashauri yetu iweze kukusanya vizuri, Hivyo mnayo nafasi ya kuwasimamia Watendaji wa Serikali huko mlimpo kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uadilifu, usimamizi bora na umakini.” Amesema Mwenda
Utaratibu huu ndio uwe muelekeo wetu wakwanza kuhakikisha Halmashauri hii inapaa katika nyanja ya mapato kwa sababu vyanzo vyote vya mapato vipo na vinaweza kuleta mapato stahiki.
“Ndugu zangu! kipimo kikubwa cha kitaifa cha utendaji wa Halmashauri yetu ni kukusanya mapato,hivyo tukawe wakali kusimamia kukusanya mapato” amesisitiza
Akiongea katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Innocent Msengi alisema kuwa kupitia watumishi wa Serikali waliopo watahakikisha wanasimamia shughuli za maendeleo na kukusanya mapato.
Aidha aliongeza kuwa Baraza la madiwani limedhibitisha kazini watumishi 13, huku watumishi wawili wakiachwa katika kipindi cha matazamio.
“Kwa sababu tumeyagundua mapungufu ya kukusanya mapato kwenye robo ya kwanza, sasa tutasimamia vyanzo visivyokuwa na msimu na kuhakikisha robo ya pili tunavuka asilimia 50 ya ukusanyaji wa mapato.” Ameahidi Msengi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani hapo, Samwel Joel amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi ambazo ameiletea Halamashauri hii ili kutekeleza miradi mbalimbali.
“Niwaombe Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wote kusimamia miradi hii sawasawa ili thamani ya fedha ilingane na miradi inayotekelezwa.” Amesema Joel na kuongeza kuwa
“Tuisimamie miradi hiyo ili tija ionekane kwa namna ambavyo Serikali ilivyokusudia.”
Baraza la Madiwani limemaliza kikao chake cha robo ya kwanza na kuahidi kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani hapo.
MWISHO
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi katikati akiongoza Barala la Madiwani robo ya kwanaza mwaka wa fedha 2021/2022. Kulia ni Makamu Mwenyekiti Ndugu Monica na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Maziku. Picha na Hemedi Munga
Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo. Picha na Hemedi Munga
Baadi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia kwa makini Baraza la Madiwani liliofanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo.Picha na Hemedi Munga
Baadi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia kwa makini Baraza la Madiwani liliofanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo.Picha na Hemedi Munga
Baadi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia kwa makini Baraza la Madiwani liliofanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo.Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.