Wanamichezo Iramba wamuenzi Hayati Mwl Julius Nyerere kwa mchezo wa mpira wa miguu ………. 01
Na HEMEDI MUNGA IRAMBA
Jumatano Okotoba 14, 2021
Singida - Iramba. MKUU wa Wilaya ya Iramba,
Suleiman Mwenda ameahidi zawadi ya Tsh milioni mbili (2,000,000) kwa timu itakayoibuka mshindi wa ligi ya Wilaya inayotarajiwa kutimuwa vumbi kabla ya msimu wa kilimo mwaka huu.
Mwenda ametoa ahadi hiyo leo Jumatano Oktoba 13, 2021 katika viwanja vya Mabatini mjini hapa wakati wa kumbukizi ya kifo cha Hayati Mwl. Julius K. Nyerere aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea na timu ya Mputu FC, Bidder FC na lukuki ya Mashabiki waliofurika katika viwanja hivyo kushuhudia mtanange kati ya timu hizo, Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza Wachezaji hao kwa kumuenzi Hayati Mwl. J.K. Nyerere kwa mchezo wa mpira wa miguu kwa sababu yeye ndie muasisi wa michezo nchini Tanzania. Ambapo Mwal. J. K. Nyerere alikuwa mahiri katika mchezo wa bao na kupendelea taifa la wanamichezo ya aina mbalimbali.
Pia amewataka wanamichezo hao kufahamu kuwa michezo sasa sio tu kiburudisho bali ni ajira inayoweza kuwakuza kuichumi, kiutamaduni na kijamii.
Kufuatia hali hiyo, Mwenda amewaahidi kuwatafutia majukwaa mbalimbali yatakayo wezesha vipaji vyao kutambulika na kuweza kutoa mchango wao kwa timu zinazoshiriki lingi mbalimbali ndani ya Tanzania ikiwemo Taifa Staa kwa sababu vipaji wanavyo.
Akiongea baada ya mtanange huo kwisha, Mkuu huyo wa Wilaya amewaahidi kuwa ofisi yake iatasaidia Tsh laki tatu (300,000) kwa ajili ya kushiriki ligi itakayoendeshwa na AZAM (Azama Confederation Cup) ili wachezaji hao wakaoneshe viwango na vipaji vyao na kuweza kujipatia fursa katika timu mbalimbali.
Akisoma risala ya wachezaji hao mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya Kocha wa timu hiyo, Christopher Mapunda amemuhakikishia Mkuu huyo kuwa anatimu ya kujivunia.
Mpunda amefafanua kuwa wamekuwa wanadumisha timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kudumisha afya, upendo na kutoa ajira kwa wachezaji kujiunga na timu zinazoshiriki ligi mbalimbali Tanzania.
Aidha amebainisha kuwa timu hiyo inakabiliwa na changamoto za kutokuwa na jezi, mipira, viatu na udhamini wa kupeleka timu katika mashindano mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu na Mdau mkubwa wa michezo Wilayani hapo, Mwl. Manase Stivini amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kukubali kusaidia masuala ya michezo katika wilaya hii.
Mwl Manase amewataka viongozi wanaoshughulikia michezo katika Wilaya hiyo (IRADIFA) kubadilika na kwenda na kasi ya Mkuu wa Wilaya.
“Mimi ninamshukuru Mkuu wa Wilaya kwa umri wake kwa kuwa bado ni kijana naamini aliyoahidi atayatekeleza kwa vitendo na kukitaka chama cha mpira Iramba IRADIFA kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya katika kuinua vipaji na kuendeleza michezo ambayo ndio uhai wa Wilaya hii. Amefafanua Katibu CWT
Naye mmoja wa mashabiki aliye hudhuria bonanza hilo, Joseph Msengi ameonesha furaha yake kwa Mkuu huyo wa Wilaya kwa namna alivyoahidi kushiriki kikamilifu katika michezo.
“Ni jambo la kipekee kwa Mkuu huyo wa Wilaya haijawahi tokea, kwa kweli tumepata jembe ambalo litaipeleka mbele Wilaya ya Iramba kimichezo, hivyo natoa wito kwa Wananchi wote kumuunga mkono.” Ameomba Msengi
Hivi karibuni kutakuwa na ligi ya Wilaya itakayohusicha timu kutoka katika kila kata za Wilaya hiyo, hivyo timu zimetakiwa kuwa na maandalizi ya kutosha kushiriki ligi hiyo kabla ya kuanza msimu wa Kilimo.
Mechi iliicha kwa timu ya Mputu FC kulazwa kwa mabao sita (6) bila dhidi ya Bidder FC.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akitambulishwa na Kapteni wa timu ya Bidder FC ndugu Jaja akimtambulisha mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, B’hango lyangwa. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akiwa katikati ya Timu ya Mputu FC punde kabla ya Bonanza la kumuenzi Mwl. J.K Nyerere lililofanyika katika uwanja wa Mabatini mjini kiomboi. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akiwa katikati ya Timu ya Mputu FC punde kabla ya Bonanza la kumuenzi Mwl. J.K Nyerere lililofanyika katika uwanja wa Mabatini mjini kiomboi. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.