Hemedi Munga Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amesikiliaza na kutatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa Sekenke Namba Moja Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwenda ametatua mgogoro huo leo Jumatano Agosti 18, 2021 wakati akiwa katika ziara zake za utatuzi wa kero mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Akiongea na Wamiliki wa Leseni wa eneo hilo pamoja na Wachimbaji Wadogo, Mwenda amewataka kufahamu kuwa wao wanategemeana katika kuwendesha Mgodi huo.
Uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo unawezesha shughuli za kiuchumi kwa mama ntilie, walimaji wa mpunga wauzao kwa mama ntilie, shughuli nyinginezo pamoja na madini yanayo uzwa kutoa mrabaha kwa serikali kujipatia mapato.
Ameifafananisha hali hiyo na mnyororo ulioungana ambapo ukikatika shughuli za uchumi na ajira kwa wachimbaji zitakuwa zimesimama.
Kufuatia hali hiyo, Mwenda amewaomba wamiliki wa Leseni ya Mgodi Namba Moja kutoza asilimia mbili (2)badala ya tatu (3) waliokuwa wamewapandishia Wachimbaji wadogo kulipia klemu.
Akikifafanua kuhusu asilimia tatu ya kulipia klemu ya Wamiliki wa leseni ya Mgodi huo, kwa niaba ya Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Jeshua Nduche amewataka wamiliki hao kudumisha mahusiano mazuri na wachimbaji Wadogo.
“Ndugu zangu Wachimbaji, hili ni swala la mahusiano kuona namna bora ya kuimaliza changamoto hii hata kama mtakuwa ndani ya sheria.” Amesema Nduche
Awali akibainisha sababu iliyopelekea Wamiliki wa Leseni hiyo kutoza asilimia tatu (3) kwa klemu, Katibu wa Wamiliki wa leseni hiyo, Joseph Mnemba amesema kuwa Bodi hiyo inamalengo yakufikia uchimbaji wa kati, hivyo taratibu za uendeshaji wa leseni ya mgodi huo zinabadilika.
Sasa hakuna uadui kati ya Bodi ya Sekenke Namba Moja na Wachimbaji wadogo, wenyenacho na wasiokuwa nacho na wala Bodi hiyo haitawazarau wachimbaji hao.
Aidha amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa sababu amewapatanisha kati ya Bodi ya Mgodi huo na Wachimbaji hao.
Kwa upande wake mmoja wa Wachimbaji wadogo wa Mgodi huo, Maduhu Lameki amewataka Wamiliki wa Leseni ya Mgodi huo kudumisha kauli nzuri kwa Wachimbaji wadogo.
Mgogoro kati ya Wachimbaji Wadogo na Wamiliki wa Leseni ya Mgodi huo uliibuka baada ya Wamiliki hao kupandisha asilimia ya kulipia klemu kutoka kwenye asilimia Mbili (2) hadi tatu (3).
Ikiwa ni siku chache tu, tangu Mkuu wa Wilaya hiyo aliporudisha rasmi shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa Sekenke Namba Moja uliokuwa umefungwa tangu mwaka 2019.
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.