Hemedi Munga, IrambaDC
Iramba. Mkuu wa wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amesikiliza na kutatua kero za wananchi mbele ya Kiongozi wa wakimbiza mwenge kitaifa ndugu, Mzee Mkongea Ali.
Akisikiliza na kutatua kero za wananchi leo Agosti 25, 2019 wakati wa kukimbiza mwenge kijiji cha Misigiri wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Akiwasilisha kero na kuomba ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Wilaya Luhahula, Mkazi wa Misigiri anayejulikana kwa jina maarufu la Mama Tururamba amesema kuna mwingiliano unaokuja kutoka TARURA kuwaondoa vijana waliobuni mradi wa kulinda magari, wakihofia vijana kupoteza ajira zao na kurudi kwenye hali yao ya zamani inayohatarisha eneo hilo kwa udokozi.
Akijibu kero hiyo Mkuu wa Wilaya, Luhahula amesema ni kweli serikali kupitia TARURA walitangaza kukusanya mapato yote yanayotokana na paki ya magari kwa hiyo tarura watakaa na wataalam kujadiliana namna bora ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.
“Ni kweli kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa serikali kupitia TARURA walitangaza kukusanya mapato yatokanayo na paki za magari, ukusanyaji wa maduhuil haya TARURA watakuja wakae na kamati ya usalama ya wilaya pamoja na wataalam tuone mfumo mzuri wa ukusanyaji wa mapato hayo, aidha atakaye jihusisha na wizi tutamkamata. “ aliongeza Luhahula
Naye Yoweri Shango akiwasilisha kero yake amesema wakati wa uchaguzi Mh, Rais John Pombe Magufuli alituahidi kutoa mikopo Sh50 milioni kwa kila kijiji imeishia wapi? huku akitaka kufahamu kwanini ajira hazitolewi licha ya kuwa wanaendelea kuwasomesha watoto wao.
Akijibu kero hiyo Mkuu wa Wilaya, Luhahula amesema kumekuwa na shule nyingi zinazotokana na usimamizi mzuri wa serikali hii na kuwataka wazazi kuwasomesha watoto wapate elimu iwasaidie katika kutatua changamoto zao, kwa kuwa shule na vyuo vikuu vimekuwa vingi, hata leo Mh Rais akitamka kwamba walioko kwenye ajira anawafuta ili aajiri tena bado hawataisha.
‘’Tunasomesha vijana wetu akiwemo na wakwangu ili waweze kujitgemea nakujua namna ya kukabiliana na maisha yao.” Alisema Luhahula
Huku akijibu suala la mikopo kuwa inawezekana mikopo hiyo inakuja kwa mfumo wa kuwezesha maendeleo na kwakuwa ilani ya CCM inaisha baada ya miaka mitano kwa hiyo muda bado haujaisha.
‘’ Leo Iramba tumejenga kituo kikubwa cha afya Ndago na Kinampanda na zimeletwa pesa nyingi katika shule zetu na Mh, Rais John Pombe Magufuli.“ Aliongeza Luhahula
Naye Helana Mtigi mkazi wa kijiji cha misigiri mtaa wa msimbazi ameomba kupitia Mwenge wa Uhuru apate ufumbuzi kuhusu kero yao watu 15 ya kutolewa upande wa kasikazi mwa kijiji hicho tangu mwaka 2010 kupisha mradi wa umeme ambapo mpaka sasa hawajalipwa, kuwa ni lini sasa watalipwa?
Luhahula amejibu kero hiyo kuwa wamelifanyia kazi kwa kutoa notisi ya kufuta hati miliki ili hawa wananchi wapate haki yao na tumeisha peleka kwa kamishna wa ardhi ili waweze kufuta.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amemuomba mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndugu Ali, kufikisha salama zao kwa Mh, Rais John Pombe Magufuli kwa kuwapendelea kuwapa miradi mikubwa karibuni katika kila tarafa kuna mradi unaendela.
Akihutubia Kiongozi wa mbio za mwenge kitafa Ndugu Ali, amemsifu Mkuu wa Wilaya Luhahula kwa kuwapa wananchi nafasi ya kumuuliza maswali ya papo kwa hapo yanayohusu maendeleo, jambo ambalo hakuna yoyote amefanya tangu waanze kuukimbiza Mwenge wa Uhuru 2019.
Akieleza namna ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwenge wa Uhuru 2019 ni kuchapa kazi bila kuchoka, kuendelea kupambana na adui ujinga maradhi na umasikini na kuendelea kuwashajihisha wananchi kuchangia kodi kwa ajili ya mapato ya Taifa letu. Aliongeza Ali
Ali amefikisha ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 kwa wananchi kuwa ni dira na muelekeo wa Taifa letu ambao umejikita katika sekta ya maji na uchaguzi wa serikali za mitaa chini ya kauli mbiu isemayo maji ni haki ya kila mtu tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kuendeleza mapambano zidi ya rushwa chini yakauli mbiu isemayo kataa rushwa jenga Tanzania, maambukizi ya VVU, UKIMWI chini ya kauli mbiu isemayo pima, jitambue, ishi. Malaria chini yakauli mbiu isemayo mimi niko tayari kutokomeza malaria we je .
Huku akiomba ushirikiano chini yakauli mbiu isemayo tujenge maisha yetu, jamii yetu na utu wetu bila madawa ya kulevya .
Mwenge wa Uhuru wilayani iramba umekimbizwa kilometa 142.5 hadi eneo la makabidhiano wilayani Igunga , umepitia Tarafa 3 , kata 7 na vijiji 14 huku ukipitia miradii 4 na shughuli sita ambapo miradi yote na shughulizi zote inajumla ya garama ya Sh1.1 bilion .
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.