Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amekabidhi mradi wa maji kijiji cha Mlandala kata ya Urughu Tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoa wa singida.
Mhe: Emmanuel Luhahula ameongozana na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Wilfred J. Kizanga (Diwani wa CCM kata ya Tulya), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl Linno Mwageni, waandisi wa maji ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida, waandisi wa maji wa wilaya ya Iramba na wataalamu mbalimbali katika kukabidhi Mradi wa maji wa Shilingi T.sh 578,498,580/=, Katiba na Hati ya usajili wa jumuiya ya watumia maji MWANGAZA Kijiji cha Mlandala kata ya Urughu wilayani Iramba.
Mhe: Emmanuel Luhahula amesema kuwa Mradi huo umekabidhiwa katika mikono salama hivyo wakazi wa Mlandala wanaopata shida ya Maji kwa muda mrefu wategemee huduma safi za maji saa 24.
Ameongeza kusema jukumu lao ni kuhakikisha wakazi wa Mlandala wanapata maji hivyo wananchi watoe ushirikiano katika kutunza miundo mbinu iliyopo na kutoa taarifa pindi wanapoona bomba linavuja.” Nimekabidhi mradi huu wa maji katika mikono salama hivyo wakazi wa Kijiji cha Mlandala watapata huduma ya Maji safi na salama. nimatumaini yangu kwamba kasi ya magonjwa yatokanayo na Matumizi haba ya maji yatapungua, utoro wa wanafunzi shuleni utapungua unaosababishwa na muda mwingi kutumika kutafuta maji mbali na makazi wanakoishi alisema Luhahula.
Akisoma Taarifa ya Mradi wa maji Mwandisi Athuman Mkalimoto alisema Mradi huu umetekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Iramba na umekabidhiwa kwenye jumuiya ya watumiaji maji MWANGAZA Kijiji cha Mlandala ya kata ya Urughu.
Lengo la mradi ni kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Mlandala huduma ya maji safi na salama pamoja na kuboresha Afya na kuinua shughuli za kiuchumi za Wananchi.
Huduma ya mradi wa maji katika kijiji cha Mlandala ilitokana na wananchi wa kijiji cha hiki kuchagua kuwa ni kipaumbele chao, hivyo waliamua kuomba mradi wa maji kutokana na shida ya maji iliyokuwa inawakabili hapo awali.
Mradi ulianza kutekelezwa Juni 2014 na kutakiwa kukamilika Januari 2015, kutokana na ukosefu wa fedha Mkandarasi aliendelea kutekeleza mradi kwa kuongezewa muda kulingana na upatikanaji wa fedha hatimaye Mradi ulikamilika mwezi Disemba 2018.
Kazi zilizofanyika ni kuchimba kisima cha maji (1) kujenga tanki (1) la kusambaza maji lenye ukubwa lita 90,000,kujenga vituo (8) vya kuchotea maji vyenye jumla la koki (16),kujenga Milambo (2) ya kunyweshea mifugo,kujenga mitungi (2) ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 5,000 na lita 1,000,ufungaji wa tanki moja la plastiki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 3,000 shule ya msingi, kuchimba mtaro wa kulaza bomba wenye urefu wa mita 15,574,kujenga nyumba (1) ya mashine,kufunga pampu (1) katika kisima cha maji,kufunga Jenereta (1) inayofua umeme wa kuendesha pampu ya maji,kuwapatia mafunzo waendesha mitambo (2) na wauza maji (8),kuunda Jumuiya (1) ya watumiaji maji na kutoa mafunzo kwa jamii juu ya matumizi ya maji safi na Usafi wa Mazingira ili mradi uwe endelevu. Alisema Eng.Mkalimoto.
Mradi utawanufaisha zaidi ya wananchi 4,000 kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama karibu na makazi wanayoishi ndani ya umbali wa mita 400 kutoka mita 1500, pia mradi utanufaisha mifugo 15,607 kwa kupata huduma ya maji ya uhakika kwenye milambo miwili ya mradi iliyojengwa.
Mkuu wa wilaya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula akikabidhi mkataba na Hati ya usajili wa jumuiya ya watumia maji Kijiji cha Mlandala Kata ya Urughu Tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.