MWALIMU KIBAKAYA: TUENDELEE KUWALINDA WASICHANA NA WANAWAKE DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwalimu Rose Kibakaya wakati wa bonanza la Michezo Machi 1, 2025 kuelekea kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025.
"Wanawake wameendelea kutambua haki zao na tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa msaada wa kisheria imekuwa kimbilio la wengi". Amesema Rose Kibakaya
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii Magreth Segu Amesema idara ya hiyo inaendelea kutoa Elimu juu ya kudhibiti matendo mbalimbali ya ukatili wa Kijinsia kupitia Kampeni ya msaada wa kisheria ijulujsnyo kama Samia legal Aid.
Michezo mbalimbali ilichezwa kama Mpira wa Miguu Wasichana na wavulana, Mpira wa Pete, kukimbua na magunia, kukimbia na yai, Elimu ya ukatili wa Kijinsia iliyotolewa na SMAUJATA, pamoja na SAMIA LEGAL AID.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.