MWENGE WA UHURU 2025 WAPOKELEWA WILAYANI IRAMBA
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mheshimiwa Suleiman Yusuph Mwenda, amepokea Mwenge wa Uhuru 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mheshimiwa Moses Machali, leo tarehe 21 Julai 2025, katika viwanja vya Shule ya Msingi Tyegelo tayari kwa kuanza mbio za mwenge katika Wilaya ya Iramba.
Katika ziara hii, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa umbali wa kilometa 87.7, na utaweka mawe ya msingi pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.
Miradi hii inatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika kuboresha huduma za jamii na kuimarisha maendeleo ya wananchi wa Iramba kwa ujumla.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni
"JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU"
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.