MWENGE WA UHURU WAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UKARABATI SHULE YA MSINGI LUONO – IRAMBA
Mwenge wa Uhuru umetembelea na kukagua shughuli za ukarabati katika Shule ya msingi Luono iliyopo wilayani Iramba. Ukarabati huo umegharimu jumla ya Shilingi 65,000,000 zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ukarabati wa vyumba 6 vya madarasa, ukamilishaji wa maboma 2 ya madarasa ya muda mrefu, ukarabati wa ofisi 2 za walimu, pamoja na uwekaji wa samani mpya (madawati na meza).
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndugu lsmail Ali Ussi, Julai 20, 2025 amepongeza mradi huo.
Mradi huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa, hali ambayo ilikuwa changamoto kubwa kwa shule hiyo. Kwa kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia, mazingira ya shule yamekuwa rafiki zaidi kwa walimu na wanafunzi, jambo linalotarajiwa kuongeza ufanisi wa utoaji wa elimu na kiwango cha ufaulu.
Wanufaika wakuu wa mradi huu ni wanafunzi wa shule ya Msingi Luono, walimu, pamoja na jamii kwa ujumla. Mradi huu unaakisi juhudi za serikali na wananchi katika kuinua kiwango cha elimu kupitia uwekezaji katika miundombinu bora. Ukarabati huo utachagiza kuendelea kutoa elimu bora katika mazingira salama, tulivu, na yanayovutia zaidi kwa maendeleo ya kitaaluma.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.