Hemedi Munga. Irambadc
Iramba. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tiyosera ameusifu uwongozi wa hospital ya wilaya kwa hatua iliyofikia ya ujenzi wa jengo la macho hospitali ya Wilaya ya Iramba.
Tiyosera ameyasema hayo leo Septemba 06, 2019 hospitali ya Wilaya ya Iramba wakati wakiwa katika ziara ya kamati ya fedha na mipango wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania.
Akisoma taarifa mbele ya kamati ya fedha na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mratibu msaidizi wa huduma za macho Lydia Sulle amesma, jengo la kliniki ya macho linajengwa kwa ushirikiano wa Sightsever na Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Jengo la macho lililojengwa hospitali ya wilaya ya Iramba limegharimu Tsh 60.3milioni, huku mdau Sightsever ametoa Tsh 46.5milioni na Halmashauri ya Wilaya Iramba imetoa Tsh 13.8Milioni. Aliongeza Sulle
Vifaa vya kufanyia upasuaji wa macho, madawa na miwani kwa ajili ya kutoa huduma vimekwisha nunuliwa na mdau akishirikana na Halmsahuri ya wilaya ya Iramba. Alisema Sulle
Akichangia katika ziara hiyo Makam Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Samwely Shilla amemtaka kaimu Mganga Mkuu, Daktari Timothy Sumbe kuandika majina kwa lugha ya Kiswahili chini ya lugha ya kingereza katika vibao vilivyobandikwa milangoni.
Hali hiyo itawasaidia wagonjwa wa macho kuweza kusoma kwa haraka na kutambua ni kwa daktari gani wanakwenda, huku kufanya hivyo ni kuitukuza na kuikuza lugha yetu ya Taifa. Aliongeza Shilla
Naye Kaimu Mganga Mkuu, Sumbe amesema vibao ambavyo vitakua na lugha zote mbili vitaletwa ili kuwarahisishia wagonjwa kutambua wanapotakiwa kuingia.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,Emmanuel Makwaya amewataka watendaji kuwa na taarifa za kina za kila mradi unaotekelezwa katani.
Huku akiwataka watendaji wakata kuwashirikisha wananchi ipasavyo katika miradi yote inayotekelezwa katika kata zao. Aliongeza Makwaya
Ziara ya kamati ya fedha na mipango imetembelea miradi inayotekelezwa kata ya Tulya na Old Kiomboi Wilayani Iramba
Ziara hiyo imeishia eneo la Salala ambalo lilikua likitumika kulea mifugo tangu mwaka 1976.
Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tiyosera na wamwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Iramba Emmanuel Makwaya wakisikiliza taarifa wakati wa ziara ya kamati ya fedha na mipango shule ya sekondari Tulya. Picha na Hemedi Munga
Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Simion Tiyosera, kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti Samwely Shilla na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Huduma za jamii Iramba Wilfred Kizanga. Picha na Hemedi Munga
Wajumbe wa kamati ya fedha na mipango wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Simion Tiyosera wakiwa katika Maogesho ya mifugo Salala wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.