Na Hemedi Munga
Singida - Iramba. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida, Innocent Msengi amewaagiza watendaji wa kijiji cha Doromoni, Afisa Uvuvi na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato katika Ziwa Kitangiri.
Msengi ametoa agizo hilo leo Alhamisi Aprili 21, 2022 wakati alipofanya ziara katika Ziwa Kitangiri akiwa na Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala wa Halmashauri hiyo katika kijiji cha Doromoni wilayani hapa.
“Niombe sana tusimamie mapato haya maana sintahitaji kuona tunafeli katika Ziwa hili kuhusu ukusanyaji wa mapato.” Aliagiza
Aidha, aliongeza kuwa hichi ni chanzo cha mapato ndani ya Halmashauri, hivyo kuanzia ngazi ya kijiji shirikianeni katika kukusanya mapato yanayopatikana kupitia samaki wanaotoka katika Ziwa Kitangiri.
“Ninahitaji katika vikao vyangu vya Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala nione taarifa inayoonesha kunamabadiliko chanya ya kukusanya mapato toka katika Ziwa hili.” Aliagiza
Halikadhalika, Msengi amemuagiza Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo, Aminiel Kamnde kuhakikisha kila eneo la kukusanyia mapato kuna kuwa na vifaa vya kukusanyia mapato (Point of Sell) vya kielektroniki.
“Siitaji kuona hili Mweka Hazina, nahitaji kuona maeneo yote yana POS ambazo zinafanya kazi kwa sababu wewe ni Mweka Hazina ulieaminiwa, hivyo timiza wajibu wako.” Aligiza
Akijibu hoja ya Diwani wa kata ya Mbelekese wilayani hapa Omari Shabani aliyetaka kufahamu kuwa ni kwa nini samaki ni wachache wakati ziwa lilikuwa limefungwa na kufunguliwa Aprili mosi. Afisa Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Deogratius Isagala alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wavuvi wasiokuwa waaminifu wakitumia nyavu za timba zenye sumu ambazo zinadaiwa kuathiri uzajilishaji wa makulia ya samaki.
Aidha, aliongeza kuwa sababu nyingine zinazopelekea samaki kutopatikana kwa wingi ukilinganisha na msimu uliyopita ni kwa sababu Ziwa limefunguliwa hivi karibuni na kiwango cha maji ni kidogo.
Pia, uwepo wa madai ya shunguli za kibinaadamu za uunganishaji wa mifereji toka katika Mto Manonga eneo la Masakaliwa Igunga ambao unaaminika kuwa ni chanzo kikubwa kinachochangia maji kuingia kwa kasi katika Ziwa Kitangiri.
Halikadhalika kupungua kwa kina cha maji kumesababishwa na upungufu wa mvua uliotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mmomonyoko wa udongo uliosababishwa na ukataji ovyo wa miti katika maeneo yanayozunguka rasilimali ya Ziwa.
Akongea katika Ziara hiyo mjumbe wa Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala Diwani wa Kata ya Kaselya wilayani hapa, Juma Makwaula alishauri kuwa Idara ya Uvuvi ihakikishe kuwa kunakuwepo mikakati inayosaidia na kukataza uharibifu kando na ndani ya Ziwa ili kulinda Ziwa Kitangiri.
“Ni vyema sasa kuwepo na mikakati madhubuti ya kudhibiti wanaochimba mitaro toka Mto Manonga na wanaolima kuziwiliwa ili kudhibiti uharibifu utakaosababisha Ziwa Kitangiri kukosa maji na Samaki kutopatikana.” Alishauri
Wakiongea kwa nyakati tofauti na mwandishi wetu wakazi wa kando mwa Ziwa Kitangiri walishauri kuwa hatua madhubuti zinapaswa kuchukiliwa ili kukabiliana na wimbi la kukosa samaki toka katika Ziwa Kitangiri.
Kwa upande wake Chazi John alisema kuwa ikiwa kutakuwa na udhibiti katika Mto Manonga na kudhibiti uwepo wa nyavu haramu utachangia kupatikana samaki wengi.
Naye Umoja Jeshuwa wakala wa kukusanya ushuru wa samaki katika Mwalo wa Doromoni katika Ziwa hilo, alishukuru upatikanaji wa samaki ambao umekuwa ukiboresha afya zao na kukuza uchumi wao.
Ziwa Kitangiri ni moja ya rasilimali muhimu iliyopo wilayani Iramba. Zipo shughuli za uvuvi zinazotoa mchango mkubwa wa kuboresha lishe ya jamii, usalama wa chakula, chanzo cha mapato ya Halmashauri hiyo, kukuza uchumi wa kipato cha kaya, kuboresha maisha na maendeleo ya mwananchi na Taifa kwa ujumla ili kufikia malengo ya kufika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
MWISHO
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida aliyevaa suti, Innocent Msengi akifafanua jambo wakati alipofika aikiwa na Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala kutembelea miradi ya maendeleo katika kata ya Kidaru kijiji cha Tyegelo Aprili 21, 2022. Picha na Hemedi Munga
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida aliyevaa suti, Innocent Msengi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba walipotembelea Ziwa Kitangiri kujionea shughuli za Uvuvi Aprili 21, 2022. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.