By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, Simion Tiyosera amewataka madiwani kukemea swala la mimba za watoto wa shule katika maeno yao.
Tiyosera ameyasema hayo leo Jumanne Desemba 17, 2019 wakati akifunga kikao cha baraza la madiwani katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Aidha Mwenyekiti huyo amewakumbusha Madiwani kupanda miti katika maeneo yao ikiwa ni hatuwa yakutimiza maazimio ya kikao cha bazara lililopita.
Baraza la Madiwani lilianza kwa maswali 9 ya papo kwa papo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo .
Akijibu moja ya swali lililo ulizwa na Diwani wa kata ya Ndulungu, Myonga Myonga aliyetaka kujuwa suala la redio RIKI, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, linno Mwageni amesema kulikuwa na mchakato wakuwa na vifaa vya kawaida na kuanza kujenga jengo ambapo haikuweza kusajiliwa.
“Tunaendelea kutenga kwenye bajeti kuomba fungu kupata vifaa vya kisasa na kuweza kuisajili,” aliongeza Mwageni
Hata hivyo jitihada zinaendelea kuwasiliana na wadau mbalimbali na kuandika maandiko mradi kwa ajili ya kuyauza kwa wadau ili watuunge mkono kwa ajili ya kuianzisha na kuimarisha redio. Alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewaomba Madiwani kusimamia watoto wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na uandikishaji wa darasa la kwanza na darasa la awali wanakwenda shule.
Pia Mkuu huyo amewasisitiza Madiwani kusimamia mapato ya serikali ili halmashauri iendelee kusimama.
“ Niombe sana yale ambayo tunaendelea kusimamia hasa kwenye mapato ya serikali tusimamie ipasavyo,” Alisisitiza Luhahula
Akiongea katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba,Samwel Joel ameomba ushirikiano uliopo uendelee kwa ajili ya maendeleo ya Iramba.
Joel amewaagiza Madiwani kulichukulia umakini swala la elimu na kutatua tatizo la matokeo ya shule za msingi wilayani humo.
“Iramba sio ya watoto wajinga haiwezekani ” Alisisitiza Joel
Mwenyekiti huyo amewaomba Madiwani waendelee kushirikiana kuisimamia Halmashauri na kuyapeleka mambo vizuri huku akiwataka wachukue hatuwa pale wanapoona mambo hayaendi vizuri.
Naye Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaomba Madiwani pamoja nakuwa na vikao vya itifaki ni vizuri kuwa na vikao kwa ajili ya kutathimini mwenendo wa Halmashuri huku akiwataka kujenga utamaduni wa kujuwa matatizo na kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo wao wenyewe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba akijibu swali mlele ya Baraza la Madiwani lililofanyika leo katika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba , Emmanuel Luhahula akiwakumbusha Madiwani kusimamia mapato ya serikali katika maeneo yao. Picha na Hemedi Munga
Mbunge wa Iramba Magharibi akiwakumbusha Madiwani kufanya tathimini ya kuendesha Halmashauri. Picha na Hemedi Munga Madiwani wakifuatilia Bazara katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.