Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya, amefanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha M/S Yaza investment Co. Ltd kilichopo Kata ya Ndago Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.
Katika ziara hiyo Naibu waziri amepokea taarifa ya Kiwanda cha M/S Yaza investment Co. Ltd ambacho kinauwezo wa Kusindika mbegu za alizeti kiasi cha tani 10 kwa siku, kuzalisha Mafuta tani 25 kwa siku, kuzalisha mashudu tani 75 kwa siku na kinasambaza sokoni tani 8,000 za Mafuta ya kula kwa mwaka na kutengeneza mashudu ya alizeti(sunflowers cake) kiasi cha Tani 14,000 kwa mwaka. Kiwanda kimeajiri wafanyakazi 50 wenye mikataba ya kudumu na wafanyakazi 110 ajira zisizokuwa za moja kwa moja.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha M/S Yaza investment Co Ltd. Ndg. Yusuph Amiri Nalompa amempongeza Naibu waziri na serikali ya awamu ya tano ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri na hatua sahihi za kuhakikisha Taifa la Tanzania linakuwa Taifa la viwanda.
Ndg. Nalompa alimueleza Naibu waziri changamoto mbalimbali za Kiwanda ikiwepo hali ya ushindani katika masoko, Riba kubwa katika mikopo inayotozwa na taasisi za fedha na upungufu wa Upatikanaji wa malighafi.
Mwandisi Manyanya amempongeza mkurugenzi wa Kiwanda cha M/S Yaza investment Co Ltd na manajimenti ya Kiwanda hicho kwa kutengeneza ajira kwa wananchi wa Iramba na amewahakikishia kutatua changamoto zinazokabili Kiwanda hicho.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula wakitembelea Kiwanda cha M/S Yaza investmentCo. Ltd kilichopo Kata ya Ndago Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akitoa maelekezo kwenye ziara ya kutembelea Kiwanda cha M/S Yaza investment Co. Ltd kilichopoKata ya Ndago Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na wananchi wa Wilaya ya Iramba kwenye ziara ya kutembelea Kiwanda cha M/S Yaza investment Co. Ltd kilichopo Kata ya Ndago Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.
Jengo la Kiwanda cha M/S Yaza investment Co. Ltd kilichopo Kata ya Ndago Wilaya ya Iramba Mkoa waSingida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.