Hemedi Munga, Irambadc
tehama@singidadc.go.tz
Iramba. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Sera, Uratibu na Uwezeshaji, Stela Ikupa emewaasa wanafunzi wa msingi na sekondari kiomboi wilaya ya Iramba Mkoani Singida Tanzania kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao kwa kutokujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo na kumshika mungu ili wawe na hofu yamungu itakayowafanya kuepukana na kutojingiza kwenye mambo ambayo ni kinyume na maadili.
Naibu Waziri ameyasema hayo leo Agosti 22, 2019 wakati akitembelea mradi wa timiza malengo kwa wasichana baleghe na wanawake vijana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Akiongea na wasichana na wanafunzi hao amewataka kutokujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo yakayowasababishia kupata mimba, kukatisha ndoto zao na kupata maambukizi ya ukimwi. Aliongeza Ikupa
Hayo yamekuja wakati akisikiliza taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi wa timiza malengo kwa wasichana baleghe na wanawake vijana unaotekelezwa wilayani Iramba uliopata ufadhili kutoka Mfuko wa Dunia kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) na athari za UKIMWI kwa wasichana baleghe na wanawake vijana nchini kutoka Januari, 2018 mpaka Desemba, 2020.
Akisoma taarifa fupi ya Mradi Mratibu wa TASAFU Wilayani Iramba, Adam Msangi amesema lego la mradi ni kuwasaidia wasichana walioko shuleni kuendelea na kuhitimu masomo yao na kufikia ndoto zao wakiwa salama dhidi ya VVU na UKIMWI.
Msangi aliongeza kuwa mradi huo unawahusu pia wale walio nje ya mfumo wa elimu kupata stadi za maisha ikiwemo ujasiriamali na kupewa mtaji utakaowawezesha kuanzisha miradi ya kiuchumi ili kujikimu kimaisha wakiwa salama dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Mpaka sasa wasichana 2,730 katika vijiji 50 vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAFU) Wilayani Iramba walinufaika na mradi. Alisema Msangi
Ambapo wasichana walionufaika na mradi huo walio ndani ya mfumo ni 1,372 huku wale walio nje ya mfumo wa shule ni 1,358.
Akibainisha walengwa hao wamekwisha patiwa Tsh140 .7milioni katika awamu mbili za Novemba, 2018 na Februari, 2019 ili ziwasaidie kupata madaftari, kalamu, sare za shule pamoja na vifaa vingine muhimu vya kujisomea na kujifunzia.
Akitoa ushuhuda Rosemary Shani kwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe, Rais John Pombe Magufuli pamoja na wadau mbalimbali kama vile TACAIDS kwa kuwakumbuka wasichana ambao ni kundi muhimu.
Ameongeza kuwa amenufaika kwa kupata mafunzo ndani ya Mkoa wa Singida yanayohusu afya ya uzazi, jinsi ya kujikinga na magonjwa ya ngono pamoja na UKIMWI, Stadi za maisha na jinsi ya kuepuka unyanyasaji wa kijinsia vilivyo muwezesha kujikinga na mimba za utotoni na magonjwa ya ngono.
Kupitia mafunzo hayo aliweza kuwaelimisha mabinti zaidi ya 500 waliopo ndani na nje ya kata katika maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi
kupitia njia ya kupata ujumbe mfupi unaoweza kuwapa elimu kuhusu afya ya uzazi na kujiepusha na tabia hatarishi. Alisema Shani
Kwa upande wake mwanafunzi wa sekondari ya New – Kiomboi kidato cha tatu Wilayani Iramba , Loyce Juma ameshukuru kuanzishwa kwa mradi huu ambao umemuwezesha kutimiza mahitaji yanayotakiwa kwa muda kama vile daftari na sare za shule .
“Mradi huu umeniwezesha kutimiza mahitaji yangu muhimu kwa mda unaotakiwa na kufanya nipate elimu ya afya, kujitambua mimi ni nani na kujithamini katika jamii na kiuchumi, kuepukana na vishawishi vya kujiingiza katika mahusiano katika umri mdogo, kupata taulo za kike na kua jasiri ninapokuwa shuleni kwa kuniongezea umakini wakati wa hedhi’ Alisema Loyce
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amemshukuru mhe, Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada anazoendelea kuzifanya kwa ajili ya kuliendeleza Taifa Letu.
Amewataka walimu wa shule za msingi, Sekondari na wanufaika wote wa mradi huu kuendelea kujifunza na kuyachukua yote yalifundishwa hapa kwenda nayo ili kutambua Taifa letu kwa sasa liko wapi na sasa tunatakiwa tujenge misingi ya namna gani liende wapi. Aliongeza Linno
Mradi wa timiza malengo kwa wasichana baleghe na wanawake vijana Tanzania unatekelezwa katika Wilaya 10 ambazo ni Kilombero, Ulanga na Malinyi Mkoa wa Morogoro, Mpwapwa, Kongwa, Bahi na Kondoa Mkoa wa Dodoma, Iramba, Singida MC na Singida DC Mkoani Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.