Naibu waziri wa afya, jinsia wazee na watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) amefanya Ziara ya Kikazi wilaya ya iramba.
Mhe; Dkt Faustine ametembelea hosipitali ya wilaya Kiomboi kwa ajili ya kujiridhirisha na hali ya huduma na upatikanaji wa Dawa.
Dkt. Ndungulile alizungumza na Watumishi wa afya hosipitali ya wilaya Kiomboi kuwa lengo la ziara hiyo ni kujiridhisha na changamoto za dawa katika hosipitali hiyo.
Hosipitali yenu inadawa zote muhimu isipokuwa kuna upungufu wa vifaa tiba na tatizo hilo litafanyiwa kazi mara moja alisema Dkt Ndungulile.
Aidha aliwataka Kaimu mganga Mkuu na Mfamasia wa hosipitali ya wilaya Kiomboi kuboresha upokeaji, utunzaji wa dawa pindi zinapoingia kwenye stoo zao na usimamizi mzuri wa dawa hizo.
Alipongeza sana hosipitali ya wilaya Kiomboi Kupata zawadi (tuzo) ya BRN kama hosipitali kwa kupata nyota 4.
Dkt Ndungulile akizungumza na Watumishi wa hosipitali ya wilaya Kiomboi aliwaasa watumishi kutoa huduma kwa kuzingatia weledi na kuwajibika katika nafasi zao kwa kutokuwa na ubaguzi kwa Wananchi tunaowahudumia.
Aidha ameongeza kusema kuwa watumishi hao wanatakiwa kuzingatia mkataba wa huduma kwa mteja pale wanapohudumia wateja na kushughulikia kero za wananchi kwa wakati.
Hospitali ya Wilaya Kiomboi ni moja kati ya vituo 33 vya serikali vya kutolea huduma za afya Wilaya ya Iramba. Ilianza rasmi mwaka 1933 ikiwa chini ya usimamizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT).Ilifunguliwa rasmi mwaka 1967 na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwaka 1972 Hospitali hii ilikabidhiwa rasmi Serikalini, na tangu wakati ule imekuwa chini ya usimamizi wa Serikali. kwa sasa inahudumia wakazi 236,282 wa wilaya ya Iramba.
Kaimu mganga mkuu Dakt Hussein Sepoko wa Hospitali ya wilaya Kiomboi akisoma taarifa ya hospitali ya wilaya (kiomboi) kwa Naibu waziri wa afya, jinsia wazee na watoto Mhe: Dkt Faustine Ndugulile (Mb) wakati wa ziara yake wilaya ya iramba amesema hosipitali inatoa huduma za mama na mtoto, huduma za wagonjwa wanje na ndani, huduma za maabara, Huduma za Afya ya akili, huduma za upasuaji mkubwa na mdogo, afya ya kinywa na meno, huduma za kifua kikuu na ukoma, tiba na matunzo kwa watu waanaoishi na VVU (CTC), Huduma ya uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi, huduma ya kinga na huduma ya radiolojia.
Ameongeza kusema Mahudhurio ya wagonjwa katika hospitali yetu ni wastani wa wagonjwa 80 hadi 120 kwa siku. Vyanzo vikuu vya mapato katika Hospitali yetu ni Bima ya Afya (NHIF) , Papo kwa papo, DRF ,fedha ya ruzuku (OC) na Fedha za Mfuko wa pamoja (BF)
Hospitali inakusanya mapato kwa kutumia mfumo wa GOT-HOMIS ambao umeonyesha mafanikio makubwa katika kukusanya mapato ambapo kabla ya mfumo kwa siku moja Hospitali ilikuwa inakusanya wastani wa kati ya Tsh 100,000 - 200,000 baada ya mfumo kwa sasa Hospitali inakusanya wastani Tsh 400,000 – 500,000 kwa siku. alisema Dkt, Sepoko.
Dkt Sepoko alieleza Mikakati ya Hospitali kupunguza vifo vya mama na watoto.
Halmashauri yetu ilipokea pia jumla ya Tsh 800,000,000 za fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya Afya 02 ambavyo ni Kituo cha afya Ndago na Kinampanda. Fedha hizi zilipokelewa tarehe 21/12/2017 na ujenzi ulianza rasmi tarehe 12/02/2018 na unatazamiwa kukamilika tarehe 30/10/2018.Kwa sasa asilimia ya ukamilishaji ni 95%.Alisema Dkt Sepoko.
Dkt Sepoko alisema Halmashauri yetu inatekeleza sera ya taifa ya uchangiaji wa huduma za afya kupitia CHF. Kwa kipindi cha muda mrefu wilaya hii imesifika kuwa na wanachama wengi wanaojiunga na CHF. Asilimia 80% ya kaya katika Wilaya ya Iramba iliwahi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) tangu kuanza kwa mfuko huu hadi sasa. Makusanyo ya mfuko huu yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka kama ifuatavyo. 2014 (Tsh 80m) 2015 (Tsh 110m) 2016 (430m) 2017 (220m) na mwaka 2018 kuanzia januari hadi Septemba (140m) zimekusanywa. Sababu za kupandisha makusanyo haya ni kuhakikisha fedha hizi zinafanya kazi ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma.
Aliongeza kusema Katika utoaji wa huduma za afya Halmashauri imeendelea na zoezi la utambuzi wa wazee ili waweze kupatiwa huduma mbalimbali za Afya. Katika kipindi cha miaka minne wazee 2,850 walitambulika na kupewa kadi za matibabu za CHF.
Dkt Sepoko ameongeza kusema, Hosipitali ya wilaya ya Kiomboi imepata mafanikio mbalimbali yakiwemo.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe; Emmanuel Luhahula ameshukuru sana serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Mhe: Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kutupatia shilingi 800,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo viwili vya afya. Kituo cha Afya Ndago na Kinampanda, Kutuletea watumishi wa kada mbalimbali hivyo kupunguza changamoto ya watumishi iliyokuwepo na
Kutuletea gari jipya la kubeba wagonjwa (ambulance) la kituo cha afya Ndago.
Aidha ameshukuru wadau wa maendeleo ambao wapo na sisi bega kwa bega katika kuboresha huduma za afya ambao ni EGPAF chini ya ufadhili wa USAID Boresha Afya, Water Aid,SEMA, Sight Saver.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.