Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizunguka katika eneo la wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu katika eneo la mlima Sekenke Misigiri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameambatana Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe: Immanuel Luhahula, Afisa Madini Mkoa wa Singida Chone Malembo kutembelea wachimbaji wadogo wadogo na kutatua migogoro yao katika eneo la mlima Sekeke Misigiri wilayani Iramba mkoa wa Singida.
Naibu waziri stanslaus nyongo amewasili katika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa wachimbaji madini ya dhahabu uliodumu takribani miaka 3 kati ya John Rutebeka na Nabii Elia katika eneo la wachimbaji wadogo lililopo katika Mlima wa Sakenke Misigiri Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Baada ya kusikiliza kero hizo, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amewagiza John Rutebeka, Nabii Elia na Afisa Madini wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo wafike ofisini kwake Jijini Dodoma siku ya Jumatano Oktoba 16 2019 ili wakae pamoja kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kila mmoja aje na vielelezo vinavyomruhusu kuchimba madini katika eneo hilo. “Mje dodoma jumatano tarehe 16.10.2019, mje ofisini tukae kwa pamoja na tume ya madini ili tutatue mgogoro huu, kila mmoja anahaki yake” alisema Mhe: Nyongo
Mhe; Nyongo ametumia fursa hiyo kuwataka watalamu wa Madini kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo ili matatizo kama hayo yanayojitokeza sasa yasiendele kujitokeza kwani ni wajibu wao kuhakikisha kuwa migogoro baina ya wachimbaji inakwisha. “Hawajui sheria na taratibu za uchimbaji, wangekuwa wanajua sheria na taratibu, watu hawa wasingekuwa wanagombana, lazima muwaelimishe, arafu mtu anapomiliki ardhi ya juu (surface area) ajue ana haki gani, na yule anayemiliki lesseni (mineral rights) ya uchimbaji ajue ana haki gani. Na pale wanapokuwa wanagongana lazima tuwasaidie na lazima tuwasaidie wanaoomba lesseni za uchimbaji, mtu ameona eneo lake linamadini anataka kuomba lesseni, anapokelewa na afisa wa madini lakini hawamuelekezi na kumsadia. Hizo lesseni zisitoke kwanza hadi mgogoro huu umetatuliwa”, Alisistsiza Mhe: Nyongo.
Naibu Waziri Nyongo, amemtaka Nabii Elia aachane na uchimbaji wa madini karibu na nguzo za umeme anatakiwa awe mita 100 kutoka kwenye nguzo za umeme, vinginevyo atachukuliwa hatua. “Buffer area inatakiwa kuwa mita 100 hakuna kuchimba chini ya nguzo ya umeme, hatutaki disturbance ya nguzo za umeme”, alisisitiza Mhe: Nyongo
Amewataka wachimbaji wadogo wadogo kutafuta lesseni kwa kuwa kutokana na wagunduzi wengi kuchimba bila kushirikisha uongozi wa kijiji, wilaya na vyama vya wachimbaji madini wamejikuta wakitoa mwanya kwa wajanja kuomba leseni hivyo kuzalisha migogoro isiyokwisha.
Alisema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka utaratibu mzuri sana wa kumlinda mgunduzi wa madini tangu anapogundua madini hayo hadi kupata leseni.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.