Hemedi Munga, Irambadc
Dodoma. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya amesema kuwa Watanzania wako tayari kuitimiza azma ya Tanzania ya viwanda kivitendo na kinachotakiwa sasa ni kuwaongezea ujuzi na mtaji.
Mhandisi Manyanya ameyasema hayo leo Agosti 06, 2020 alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Uwanja wa Maonesho ya kilimo Nzuguni Jijini Dodoma na kukutana na mbunifu wa kifaa alichokiita pawatila kutokana na kazi kinazozifanya toka Wilayani Iramba.
“Ni wakati sasa kwa vijana wanaomaliza vyuo kutumia ubunifu huo kuwa ni funzo na fusra ya kujitegemea baada ya kupata mafunzo katika vyuo vyao” amesema Eng. Manyanya na kuongeza kuwa
“Kuna haja ya hawa wenye ubunifu walio na maono ya kubuni vifaa mbalimbali kuungana na wale waliotoka masomoni wenye maono na ujuzi wakuweza kubuni vifaa mbalimbali ili waanze kuvitengeneza.”
Amempongeza ndugu Benson Makoma kuwa mbunifu wa kifaa hicho chenye uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kulimia na kupukuchukulia mahindi kwa muda mfupi.
Akitoa taarifa fupi mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya mbunifu wa kifaa hicho, Benson Makoma amesema kuwa changamoto zilizokuwa zimemzunguka ndio chachu ya msingi iliyomfanya aweze kubuni kifaa hicho kiwe msaada wa kutatua changamoto hizo.
“Nilipo kaa na kutulia niliweza kubuni kifaa hichi ambacho kinanguvu ya kuvuta tela lenye magunia kumi na kinauwezo wa kupukuchua mahindi kiasi cha ngunia mia moja kwa masaa mawili,” amefafanua Makoma na kuongeza kuwa
“Kifaa hichi kinauwezo wa kukimbia kwa spidi nzuri na kwenye barabara ya aina yoyote.”
Amesema kuwa kumekuwa na changamoto hasa katika upatikanaji wa vifaa vya kuundia kifaa hicho katika maeneo ya karibu na hivyo kulazimika kuvifuata umbali mrefu.
“Hata hivyo vifaa vya kuchomelea sio vyakwangu mara kwa mara nimekuwa nikienda mji wa Shelui kwa ajili ya kuchomelea,” ameongeza Makoma
Akijibu swali la Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara aliotaka kujua kiasi cha gharama zilizotumika kukamilisha ubunifu huo, Mkoma amesema kuwa Kifaa hicho kimegharimu takribani Tsh 2.2 milioni ambapo mpaka sasa gharama hizo zimekwisha rudi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Jackson Masaka alihoji aina ya mafuta ambayo yanaotumika katika kifaa hicho pamoja na muda uliotumika kukibuni kifaa hicho.
Akijibu hoja hiyo, Mkoma amesema kifaa hicho kinatumia mafuta ya dizeli na kimechukua muda wa mwezi moja kukamilika.
MWISHO
Kufuatia ubunifu wa ndugu Benson Mkoma toka kata ya Mtekente Wilayani Iramba Mkoa wa Singida, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya amemzawadia fedha ili kuunga mkono juhudi zake za kutekeleza azma ya Tanzania ya Viwanda kuwa inawezekana na Watanzania wanaweza. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Marietha Kasongo akimuonesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya ubunifu wa pawatila iliyobuniwa na Benson Mkoma toka kata ya Mtekente Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Marietha Kasongo akiongozana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya katikati na wambele kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Jackson Masaka kuelekea kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya hiyo liliopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya kilimo Nzuguni Jijini Dodoma. Picha na Hemedi Munga
Mjasiriamali toka kijiji cha Doromoni kata ya Tulya Wilayani Iramba Mkoani Singida akimuonesha samaki aina ya Kamongo wanaopatikana Ziwa Kitangiri Wilayani humo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya hiyo liliyopo katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nzuguni Jijini Dodoma. Picha na Hemedi Munga
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya akionesha ubunifu wa chungu kilichobuniwa na Jawel Maganga toka Wilayani Iramba Mjini Kiomboi kikionesha kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu wakati alipotembelea banda la Halmashauri hiyo katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nzuguni Jijini Dodoma. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Marietha Kasongo akimuonesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stella Manyanya shamba darasa la alizeti liliopo viwanja vya maonesho ya Kilimo Nzuguni Jijini Dodoma. Picha na Hemedi Munga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.