Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa amewapongeza wananchi wa kijiji cha kisiriri kwa kubadilisha maisha kupitia mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF).
Mwanjelwa ameyazungumza hayo wakati wa ziara yake leo Ijuma tano Januari 8, 2020 kijiji cha Kisiriri Tarafa ya Kisiriri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Akiongea na wananchi katika ziara hiyo, amewataka kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuleta zaidi ya 120 milioni kijijini hapo huku zaidi 6.9 bilioni zimeletwa kwa wilaya nzima.
Amewaeleza kuwa Rais Magufuli amekubali mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) awamu ya pili kuendelea huku akiwahakikishia kuwa vijiji 70 vitafikiwa na mradi huo ukuilinganisha na awamu yakwanza ulionufaisha vijiji 50.
Utaratibu wa kuchaguwa kaya maskini umeboreshwa ili kuepusha uchakachuaji na itapita timu nyingine kujiridhisha kama zoezi hilo limefanyika sawasawa.
“Tutakuwa tunakuja kwenye kaya kuona kwa macho na itapita timu nyingine kujiridhisha, ” alisisitiza Mwanjelwa
Aidha amewataka kuyaishi yale wanayoyatolea ushuhuda kuwa ni tija waliyonufaika kipitia mpango wa kunusuru kaya maskini(TASAF).
Mwanzoni akisoma taarifa fupi ya Mpango wa kunusuru Kaya maskini (TASAF) mbele ya Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji, James Shani amesema mradi huo umewawazesha kutekeleza shughuli nyingi.
Shani amezitaja shughuli zilizotekelezwa kuwa ni uhaulishaji fedha za ruzuku na utimizaji wa masharti ya afya na elimu, pili ni ajira ya muda mfupi, tatu ni fedha za vifaa vya utekelezaji wa ajira ya muda mfupi huku akihitimisha na ujenzi wa miundombinu katika maeneo maalum katika sekta za afya na elimu.
Mradi huo umeweza kuwanufaisha wasichana balehe 1,372 kwa kuwapa fedha za kujikimu maisha.
Kugawa taulo za kike 8,910 kwa wasichana balehe 1,372 huku akibainisha kuwa wasichana balehe 827 walio nje ya mfumo wa shule wameweza kupata mafunzo ya ujasiriamali, uwandaaji wa mpango wa biashara katika kata 17 na vijiji 50 vilivyoko kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini(TASAF), alisema Shani.
Aidha amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa Halmashauri imechukuwa hatuwa mbalimbali za ufumbuzi wa changamoto anuwai ikiwa ni pamoja na kuendelea kuielimisha jamii kuhusu malengo na dhamira ya serikali na wadau wa maendeleo kuhusu kutoa fursa mbalimbali za kupunguza umaskini.
Akitoa ushuhuda wa kunufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini(TASAF), Esta Makala (80) amesema ameweza kununua bati 23 na kusogeza mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
Naye Upendo Mashantala amesimulia kuwa alikuwa na hali mbaya ya kukosa chakula na mahali pazuri pakulala, lakini baada ya kupewa ruzuku kupitia mpakongo wa kunusuru kaya maskini (TASAF) aliweza kununua mbegu bora zilizomuwezesha kupata mahindi na baada ya kuyauza aliweza kujenga nyumba ya bati.
Kwa upande wake Sara Kiongo amesema kuwa ameweza kunufaika kupitia mradi huo kwa kununuwa mbuzi na kulipia kadi ya CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya kulinda afya zao.
Kupitia mpango wa mafunzo ya timiza malengo yalioendeshwa kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), Lucyana Shaluwa amesema wamejifunza kujiamini, namna ya kupanga bei kulingana na mshindani wako, kuzifahamu faida na hasara na kujiepusha na makundi yasio stahili kama vile uvutaji bangi, uvutaji wa madawa ya kulevya, kuingia kwenye ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Akiongea katika ziara hiyo katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iramba, Ibrahimu Mjanaheri amemsifu Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo miradi mbalimbali.
Mjanaheri amesema Hospitali za wilaya 99 zimejengwa kwa kipindi cha miaka 4 ukilinganisha na wakati anaingia madarakani 2015 ambapo kulikuwa na hospitali 77.
Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa katikati akienda kwenye nyumba ya mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini ili kuangalia utekelezaji wake, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula wakati kushoto kwa Naibu Waziri ni Adamu Msangi Mratibu wa Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Iramba. Picha na Hemedi Munga
Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) huku kushoto kwake ni Adamu Msangi Mratibu wa Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.