By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Kilundo ni kitongoji kilichopakana na kitongoji cha shati, Shengelo na Mnguluko kata ya New-kiomboi Tarafa ya Kisiriri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania.
Wakionesha furaha ya upatikanaji wa maji kitongojini hapo, wenyeji wamesema hakujawahi kuchimbwa kisima kirefu chenye maji Kilundo.
Akiongea na Mwandishi wetu leo Alhamisi Oktoba 17, 2019 Daudi Msemembo amesema wazo la kuchimba kisima lilitokana na ndoto.
“Niliota mara ya kwanza, mara ya pili na yatatu kuwa ninachimba kisima na maji yakapatikana, ndipo nilipoamua kuchimba kisima hicho.” Alisema Msemembo
Msemembo alichimba kisima hicho maarufu kwa jina la Mkali wa Kijiji ambacho inasadikika kinaurefu takribani futi 30 kwenda chini kwa kutumia nyezo za asili kama vile sururu, jembe, beleshi na panga.
Akitoa wito kwa jamii inayomzunguka, Msemembo ameiomba jamii kumuunga mkono kwa kununua maji huku akiuza ndoo moja kwa 250 Tsh.
Kufanya hivyo kutamuwezesha kupata pesa ya kununua simenti na nondo za kujengea kisima hicho cha kwanza na kirefu chenye maji safi katika vijiji vya shati kati, shengelo na Mnguluko vinavyopakana na Kilundo.
Kujengea kisima hicho kutaiweka jamii ya watu wazima, watoto na mifugo kuwa salama na hatari ya kutumbukia kisimani hapo. Alisema Msemembo
Naye baba mzazi wa Msemembo, Daudi Mbutu amesema alifurahi alipoitwa na mwanaye kuja kuyaona maji.
Awali hakuamini kupatikana maji mahali hapo kwa kuwa alizani Msemembo anachimba choo.
“Baba njoo uyaone maji, siku ya kwanza tukachota ndoo mbili, siku ya pili tukajaza jaba.” Alisema Mbutu.
Mmoja wa majirani aliotambulika kwa jina la Neligwa Iddi amemsifu Msemembo na kumpatia jina maarufu la Mkali wa Kijiji kwa kuchimba kisima hicho chenye maji aliyoyafananisha na maji ya mtoni kwa kuwa ni meupe hayana chunvi.
Wakazi wa Kilundo wanategemea maji kutoka mto maarufu wa Kenkangombe unaomwaga maji yake ziwa Kitangiri linalopatikana Iramba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.