Ofisi ya Rais - Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kati yatoa mafunzo ya Maadili kwa Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Mafunzo hayo ya Siku Moja yamefanyikika Februari 27, 2025 katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na yametolewa na mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais - Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kati Christian Kapere.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi ametoa shukrani kwa Ofisi ya Rais - Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kati kwa mafunzo hayo ambayo husaidia kujenga ushirikiano kwa Watumishi.
"Hili jambo Lina tija sana Nina uhakika tutaendelea kuwa na ushirikiano na tutaendelea kuijenga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Amesema Msengi
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti Msengi ametoa wito kwa Madiwani pamoja wataalamu wa Halmashauri kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ungonjwa wa Kipindupindu hili likiwa ni pamoja na kuhakikisha Wananchi wanahasishwa kusafisha maeneo yao.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.