Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida Mhe:Emmanuel Luhahula Akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni wamefanya Operesheni ya kudhibiti utoro shuleni na ajira za watoto chini ya miaka 18 katika maeneo ya Migodi Wilaya ya Iramba ili Kubaini wanafunzi waliotoroka shuleni na Watoto ambao hawajapelekwa shuleni kuandikishwa.
Wamefanya Opereshani hiyo baada ya Kujiridhirisha kuwa uandikishaji wa watoto shuleni umepungua sana ikiwa Darasa la awali ni 77%, Darasa la kwanza ni 92.7% na Kidato cha kwanza ni 96%. Vile vile Mahudhurio ya Wanafunzi shuleni yamepungua Sana ikiwa sekondari ni 98% na Shule za Msingi ni 95%.
Operasheni hiyo imefanyika katika mgodi wa Zambia Kata ya Mgogo, Mgodi wa Sekenke one, Mgodi wa Namba Nne,Mgodi wa Namba Tano na Mgodi wa Mzizini Kata ya Ntwike Tarafa ya Shelui na Vijana 91 walikamatwa kutoka Wilaya Mbali Mbali za Iramba, Igunga,Bariadi, Shinyanga, Tabora, Mkalama, Ikungi, Manyara, Kishapu,Kilimanjaro,Butiama na Chato.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba ametoa Maelekezo kwa Wazazi/Walezi wa Watoto hao ambao hawajaandikishwa wapelekwe shule mara moja, Vile vile Watoto waliotoroka shule warudishwe haraka sana na Mzazi/Mlezi atayekaidi atachukuliwa hatua kali za Sheria.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.