Muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Ndg. Dijovison Ntangeki akiongozana na wataalamu wa maji amekabidhi Mradi wa maji wa Shilingi milioni 588,756,487/=, Katiba na Hati ya usajili wa jumuiya ya watumia maji (WASOWA) Kijiji cha Mgungia kata ya Kaselya Wilayani Iramba.
Muwakilishi Mkuu wa Wilaya ya Iramba akizungumza na wananchi amesema Mradi huo umekabidhiwa katika mikono salama hivyo wakazi wa Kijiji cha Mgungia watapata huduma ya Maji safi na salama. Ameongeza kwa kusema nimatumaini kwamba kasi ya magonjwa yatokanayo na Matumizi haba ya maji yatapungua, utoro wa wanafunzi shuleni utapungua unaosababishwa na muda mwingi kutumika kutafuta maji mbali na makazi wanakoishi.
Ndg. Ntangeki amesema jukumu lao ni kuhakikisha wananchi wa Mgungia wanapata maji hivyo wananchi watoe ushirikiano katika kutunza miundo mbinu iliyopo na kutoa taarifa pindi wanapoona bomba linavuja.
Ndg. Ismail Ally Ghone, Mwenyekiti wa Kijiji cha mugungia Akipokea mradi huo kwa niaba ya wananchi, ameshukuru Halmashauri ya wilaya ya Iramba kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii na kuhaidi kutuza miundo mbinu ya mradi huo.
Akisoma Taarifa ya Mradi wa maji, Mwandisi Athuman Mkalimoto alisema Mradi huu umetekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Iramba na umekabidhiwa kwa jumuiya ya watumiaji maji (WASOWA) Kijiji cha Mugungia kata ya Kaselya, Mradi ulianza kutekeleza Juni 2014 na kukamilika mwezi Novemba 2017.
Mpaka kukamilika kwa mradi huu, umetumika shilingi Milioni 588,756,487/= na shilingi Milioni 5 nguvu za wananchi.
Lengo la mradi ni kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Mugungia huduma ya maji safi na salama pamoja na kuboresha Afya na kuinua shughuli za kiuchumi za Wananchi.
Mradi wa maji katika Kijiji cha Mugungia ulitokana na Wananchi wa Kijiji hiki kuchagua kuwa ni kipaumbele chao, hivyo waliamua kuomba mradi wa maji kutokana na shida ya maji iliyokuwa inawakabili hapo awali.
Aidha mradi huo wa maji unahudumia wananchi wapatao 5,375 chenye vitongoji vitano vya Ndyala kati, Ndyala juu, Mwandu, Ugani na Msisi kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama karibu na makazi wanayoishi ndani ya umbali wa mita 400 kutoka mita 1500, pia mradi wa maji unahudumia mifugo 5,689 kwa kupata huduma ya maji ya uhakika kwenye milambo miwili ya mradi iliyojengwa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.