Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amemshukuru Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za miradi yamaendeleo mkoani humo na ameahidi ataendelea kusimamia miradi, sambamba naukusanyaji wa mapato katika Halmashauri zote saba za Mkoa huo kwa nia yakutekeleza maono ya Rais ya utekelezaji miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Serukamba akizungumza leo (tarehe17 Oktoba, 2023) Wilayani Iramba wakati wa salamu kwa Rais Dkt. Samia SuluhuHassan ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwa sikutatu Mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi, kuizindua na kuweka jiwe lamsingi kwenye miradi ya maendeleo.
Aidha, Serukamba amemuhakikishiaRais Dkt. Samia, kwamba kutokana na mambo mazuri yaliyofanywa kwa kipindi chamiaka miwili hususan katika sekta ya afya, kilimo, maji, nishati na nyingine nihakika wanasingida watalipa deni hilo kwa kuhakikisha wanamchagua kwa kishindokatika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwatangu Tanganyika ipate uhuru Rais Dkt. Samia amefanya maendeleo makubwa kwawananchi nchi nzima hususan katika Mkoa wa Singida.
Akizungumzia Wilaya ya Irambaamesema kuwa Iramba ina vijiji 70 lakini kila kijiji kina mradi mkubwa wamaendeleo jambo ambalo Rais amafanya mambo yake kwa vitendo kwa manufaa yawananchi wake.
Akizungumza kwenye hitimisho yaziara hiyo, Serukamba amesema wananchi sio kwamba wanampenda Rais Dkt. Samiakwa kuwa anatoka katika Chama Cha Mapinduzi bali anapendwa kutokana na utendajiwake bora wa kazi ambao unaonekana na wenye kugusa maisha ya watu.
Amesema kutokana na hali hiyowananchi wa Singida wana deni kwa Rais Samia na deni hilo litalipwa kwa awamumbili ambapo ni katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na deni linginelitalipwa kwa fidia mwaka 2025 kwa kuongoza kupiga kura nyingi kwa Rais, Mbungena Diwani wanaotoka katika Chama Cha Mapinduzi.
Tangi kubwa lenye ujazo wa lita 300,000 likiwa limejengwa katika Kijiji cha Kizonzo kama sehemu ya mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Mji wa Shelui tarehe 17 Oktoba, 2023
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.