By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne Oktoba 15, 2019 katibu mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa ujumla yanaonesha ufaulu umeongezeka kwa aslimia 3.78 lakini ufaulu katika somo la kingereza bado ni mdogo ukilinganisha na masomo mengine.
“ Ufaulu katika somo la kingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za maksudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hilo” amesema Dk Msonde
Kufuatia matokeo hayo shule ya msingi Kiomboi- Hospitali iliyopo Wilayani Iramba Imekuwa ya kwanza katika wilaya hiyo.
Shule hiyo iliyopo katika kundi la wanafunzi 40 au zaidi imekua ya kwanza kihalmashauri kati ya shule 66, kimkoa ya 7 kati ya 375 na kitaifa 582 kati ya 9929.
Huku nafasi ya pili kiwilaya ikishikwa na shule ya msingi Misigiri, yatatu shule ya msingi Lulumba, yanne shule ya msingi Kiomboi-Bomani na ya tano ni shule ya msingi Kidaru.
Huku kundi la wanafunzi chini ya 40 katika wilaya hiyo shule ya msingi Salala imekuwa yakwanza kati ya 22, kimkoa ya 25 kati ya 156 na kitaifa 2608 kati ya 7102.
Wakati nafasi ya pili katika kundi hilo ikishikwa na shule ya msingi Ndurumo, yatatu shule ya msingi Munkonze, ya nne shule ya msingi Motomoto na ya tano shule ya msingi Mukulu.
Huku shule ya msingi Msansao ikishika nafasi ya mwisho kiwilaya 66 kati ya 66, kimkoa 375 kati ya 375 na kitaifa 9920 kati ya 9929.
Hata hivyo shule ya msingi Ntwike na shule ya msingi sekenke hazijawekewa matokeo.
Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Muguni ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.
Kimkoa , Mkoa wa Dar es salaam umeshika namba moja, ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.