Na Hemedi Munga
tehama@irambadc.go.tz
Singida - Iramba. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida, Yohana Msita amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mhandisi Michael Matomora kwa namna anavyoshirikiana na Wakuu wa Idara na Vitengo kutekeleza miradi ya zaidi ya Tsh 12 bilioni wilayani Iramba mkoa wa Singida.
Msita ametoa pongezi hizo leo Alhamisi Machi 17, 2022 wakati akiwa na Kamati ya Siasa ya mkoa wa Singida kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) robo ya tatu Januari hadi Machi 2022 wilayani hapa.
Akiongea na wananchi waliohuduria katika miradi mbalimbali, Msita alisema kuwa wanakila sababu ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuleta zaidi ya Tsh 12 bilioni zinazotekeleza miradi ya afya, elimu, barabara na maji wilayani Iramba.
Katika hatua nyingine amewaasa wakuu wa Idara na Vitengo kushirikiana na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa sababu kila mmoja katika eneo lake analijenga Taifa.
Aidha, alitahadharisha tabia ya kucheza na mifumo ili kuchea fedha za umma.
“Ndugu zangu niwaambie kuwa tabia ya uaminifu, uadilifu na uchapa kazi wako ndio utakaokutoa hapa ulipo na kukupeleka sehemu nyingine maana haitaji sana muunganiko wako ispokua kazi yako ndio itakayokutambulisha” Alisisitiza Msita
Akiongelea ubora wa miradi iliyotekelezwa kwa kiwango stahiki kulingana na fedha iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mjumbe wa kamati ya Siasa mkoa wa Singida Diana Chilolo alisema kuwa miradi hii imeleta ukombozi mkubwa kwa wananchi hasa akina mama wajawazito.
“Hakika sisi tunaondoka tukiamini kuwa miradi hii ni msaada kwa wananchi kujipatia huduma bora na kuwafanya wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi ili Taifa letu lizidi kuenndelea.” Alisema Diana
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mhandisi Michael Matomora aliishukuru Kamti ya Siasa mkoa kwa kutembelea miradi na kuwakumbusha wao kama viongozi na kioo kwa jamii kuwa waadilifu.
“Ni kuhakikishie ndugu kiongozi kuwa sisi ni wamoja na lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa waadilifu kwa kiwango tutakakacho kiweza.” Alisema Matomora
Aidha, alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja akiwa ni Rais maana wengi walidhania kuwa hatoweza lakini Rais amefanya makubwa ambayo hayajawahi fanyika tangu kupatikana kwa uhuru, hivyo mambo hayo yanaandika historia mya katika Taifa letu.
“Kwa kweli tunashukuru Mungu amemshika na kumpingania Rasi wetu hatimaye Taifa letu linazidi kuendelea katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa.” Aliongeza
Naye Ali Rashidi mkazi wa Kijiji cha Msansao Tarafa ya Shelui Wilayani hapa alisema kuwa miradi hii imekuwa ni lulu na tunu kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Iramba, hivyo aliupongeza utawala wa Rais Samia kwa namna unavyowajali wananchi.
Kamati ya Siasa mkoa wa Singida imetembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Maluga inayojengwa kwa Tsh 470 milioni, mradi wa maji kijiji cha Zinziligi uliotekelezwa kwa Tsh 311.8 milioni, ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Mtoa kinachojengwa kwa Tsh 400 milioni na matengenezo ya barabara ya Shelui Nkyala kwa Tsh 450 milioni.
MWISHO
Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida leo Machi 17, 2022 imefanya ziara kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika kata ya Maluga wilayani iramba mkoa wa Singida. Shule inajengwa kwa gharama ya Tsh 470 milioni. Picha na Hemedi Munga
Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida leo Machi 17, 2022 imefanya ziara kukagua mradi wa maji kijiji cha Zinziligi wilayani iramba mkoa wa Singida. Mradi unatekelezwa kwa gharama ya Tsh 311.8 milioni. Picha na Hemedi Munga
Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida leo Machi 17, 2022 imefanya ziara kukagua mradi ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Mtoa wilayani iramba mkoa wa Singida. Mradi unatekelezwa kwa gharama ya Tsh 400 milioni. Picha na Hemedi Munga
Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida leo Machi 17, 2022 imefanya ziara kukagua mradi matengenezo ya barabara ya Shelui Nkyala wilayani iramba mkoa wa Singida. Mradi unatekelezwa kwa gharama ya Tsh 450 milioni. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.