By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkoa wa Singida umeshika nafasi ya 5 kwenye zowezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Uchaguzi ambao ni wa 6 tangu Nchi ya Tanzania iingie katika mfumo wa vyama vingi.
Akiongea na waandishi wa habari leo Ijumaa Oktoba 18, 2019 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amesema Mkoa wa Singida umewaandikisha watu 910,344 sawa na asilimia 90.
Uandikishaji huo umeifanya Singida kushika nafasi ya 5 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkoa wa Dar es salaam, nafasi ya pili ikishikwa na Mkoa wa Pwani, Yatatu Mkoa wa Mwanza wakati nafasi ya nne ikishikwa na Mkoa wa Tanga.
Kwa ujumla mikoa yote na Halmashauri zote zimefanya vizuri katika uandikishaji ambapo wote wamepata asilimia 65 kwenda juu. Alisema waziri
Huku akitoa zawadi ya vyeti na vikombe kwa mikoa mitano iliyofanya vizuri ambayo ni Mkoa wa Singida, Mkoa wa Tanga, Mkoa wa Mwanza, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es salaam.
Nazo Halmashauri zilizofanya vizuri katika zoezi hilo, ya tano ni Halmashauri ya Munduli, yanne ni Temeke, yatatu ni Kibiti, ya pili ni Ngorongoro na ya kwanza ni Mlele.
Aidha Waziri Jafo amesema halmashauri zilizokuwa na mzigo mzito kwa idadi nyingi ya wapiga kura yatano ni Kinondoni, ya nne ni Ubungo, ya tatu ni Jiji la Mwanza, ya pili ni Manispaa ya Ilala na ya kwanza ni Manispaa ya Temeke.
Kufuatia uandikishaji huo Waziri Jafo amewashukuru wakuu wa mikoa kwa kuingia saiti kuhamasisha kujiandikisha.
Huku akiwashukuru kwa dhati Marasi na sekretarieti ya Mikoa, Wakuu wa Wilaya na kamati zao za ulinzi na Usalama, Wakurugenzi na watendaji wote wa Halmashauri, Makatibu Tarafa na watendaji wa kata mpaka ngazi ya chini.
Aidha amevisifu vyombo vya habari vya Tanzania kwa kuwa vya mfano kwa kuonesha uzalendo wakupitiliza na kulitendea haki zoezi hilo.
Jumla ya watu walioandikishwa ni 19.7 milioni sawa na asilimia 86 ya lengo na kuweka historia ya kwanza ukilinganisha na asilimia 63 mwaka 2014. Alisema Waziri Jafo
Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura ulianza Oktoba 8, na kuhitimisha zoezi hilo Oktoba 17, 2019.
Waziri Jafo amewaomba wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi kwa kuwa maendeleo yanaanzia huko kwa kupata viongozi wazuri huku akiwaasa kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuwataka kudumisha amani ambayo ndio tunu ya Taifa la Tanzania.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.