Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Iramba imetoa Semina ya Siku Moja kuhusu Elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, Kwa Makundi ya Watu wenye Mahitaji Maalumu
Kuelekea Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025 Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Iramba imetoa semina ya Elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa Makundi yenye mahitaji maalumu.
Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na TAKUKURU Wilaya ya Iramba yametolewa Januari 27, 2025 katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na kuwashirikisha baadhi ya wawakilishi kutoka Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) ,Chama Cha Watu Wasiiona (TLB), Chama Cha Walemavu wa Viungo ( CHAWATA ), Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA)
Akizungumza katika kuhitimisha mafunzo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Bi. Bupe Mwakibete amewataka wawakilishi hao kutoka vyama vya Watu wenye Mahitaji Maalumu kuendelea kutoa Elimu kwa wenzao juu ya mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu la Kila mtu hivyo kutoa ushirikiano pindi wataksoohitajika kufanya hivyo.
"Jukumu la Mapambano ya Rushwa ni letu sote,tuhakikishe tunakuwa mstari wa mbele dhidi ya mapambano haya kuelekea kipindi hiki Cha Uchaguzi. " Amesema DAS Bupe Mwakibete.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania Bw. Nassoro Ernest Amos ameishukuru TAKUKURU kwa kutoa Mafunzo hayo kuhusu Elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 kwa Makundi ya watu wenye Mahitaji Maalumu kwani wamepata Elimu itakayowawezesha kuwa mstari wa mbele kushiriki Katika mapambano dhidi ya Rushwa.
"Tumepata Elimu itakayotuwezesha na sisi watu wenye Mahitaji Maalumu kushiriki Katika mapambano hayo kwa kuwa Rushwa ni adui mkubwa wa haki na wajibu wetu ni kuitokomeza kwa kuhakikisha tunachagua Viongozi Waadilifu ambao hawajatokana na Rushwa" Alisisitiza Nassoro Amos.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.