By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Kesho ndio siku ya mwisho ya uandikishaji wa Daftari la Wapiga kura kama ilivyokuwa imesemwa awali.
Serikali imeongeza siku tatu za mchakato huo ili kuwapa nafasi watanzania wengi kujiandikisha.
Leo Jumapili, Oktoba 13, 2019 katika mtandao wa kijamii wa Facebook wenye akaunti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi), imeweka taarifa inayoeleza kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameongeza siku tatu za uandikishaji kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura.
Hivyo uandikishaji wa Daftari la Orodha ya Wapiga Kura utakamilika Alhamisi Oktoba 17, 2019.
Akiwa mkoani Katavi Oktoba 11, 2019 kwenye ziara ya Rais wa Tanzania, John Magufuli, waziri huyo aliahidi kupeleka mapendekezo maalumu kwa Rais kuomba mikoa itakayofanya vibaya iongezwe muda wa uandikishaji.
Aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya uandikishaji wa Daftari la Wapiga kura kwenye mikoa mbalimbali.
Huku Oktoba 12, Rais Magufuli, akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za shirika la ndege la Tanzania (ATCL) mkoani Katavi, alisema mikoa ambayo viongozi wake watashindwa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili wapige kura atawashangaa huku akisema hadharani kama atalaumiwa na watanzania kwa hatua atakazozichukwa.
“ Wazairi (Jafo) ametoa takwimu za baadhi ya mikoa iliyofanya vizuri. Ninafuatilia lakini alitoa iliyofanya vibaya, mchakato ukikamilika nitataka anipe taarifa ya mikoa iliyofanya vizuri na vibaya”. Alisema Rais Magufuli kwenye ziara hiyo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.