Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Timu ya mpira wa wavu ya Watumishi wa Wilaya ya Iramba imeifunga Timu ya wavu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama seti mbili bila.
Mchezo huo umefanyika leo Jumamosi machi 7, 2020 katika uwanja wa Mabatini uliopo mjini Kiomboi.
Dakika chache baada ya kuanza kwa mchezo huo timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba walioenekana kulisakama lango la wapinzani wao huku Fabiano Nyamuhaga akionekana kuwa mwiba mpachikaji wa mabao zidi ya timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Mkalama.
Baada ya mchezo wa wavu kuisha Watumishi hao waliuanza mchezo wa mpira wa mguu katika kiwanja cha Mabatini kilichopo mjini hapo.
Mchezo huo wa mpira wa mguu ulianza kwa timu zote mbili kushambuliana kwa kasi ambapo dakika ya 11 Ashadi Abdallah anaipatia goli la kuongoza timu ya Watumishi wa Mkalama.
Mchezo ulizidi kuwa na kasi ya kushambuliana kwa zamu jambo ambalo lilipelekea timu ya Watumishi ya Mkalama kupata penati dakika ya 35 ya mchezo huo.
Hata hivyo Afisa Utamaduni wa timu ya Halmashauri ya Mkalama, Luzegele Kilala anaukosa mkwaju wa penati nakufanya matokeo kuwa Mkalama goli moja na halmashauri ya Wilaya ya Iramba bila.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika ni timu ya Watumishi wa Halamashauri ya Wilaya ya Mkalama wanaotoka wakiwa wanaongoza goli moja bila zidi ya timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakilisakama lango la timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Mkalama.
Ilikuwa dakika ya 58 ambayo Jemsi Tambue anaisawazishia timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba baadaya kupokea krosi safi iliyotoka kwa kapteni wa timu hiyo.
Mchezo huo uliongeza kasi kwa timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kulisakama lango la timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Dakika ya 78 Godfrey Sanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama anapiga shuti kali lililomshinda mlinda lango wa timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na kugonga mwamba kutoka nje.
Timu hizo zilitoshana jasho kwa mchezo mzuri hadi dakika 90 zinakamilika zikiwa zimefungana goli moja na kufanya matokeo hayo kuwa sare ya moja moja.
Kampteni wa timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mahmudu Said amesema matokeo hayo yametokana na timu kutokuwa pamoja na hivyo kupanga kikosi kwa kutumia uzowefu na kufanya kipindi cha kwanza kushambuliwa mara kwa mara na kipindi cha pili baada ya kujua kila aliyekuwa vizuri ndio maana tuliukamata mchezo.
Wanajipanga kwa kuwakusanya wachezaji ili wafanye mazoezi ya pamoja ili watakaporudiana waifunge timu ya Watumishi wa Mkalama
“ Tumeanza mazoezi ya pamoja yatakayodumu kwa muda wa wiki mbili au tatu ili tutakaporudiana na timu ya Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama tupate ushindi,” amesema Said
Naye kapteni wa timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Luzegele Kilala amesema wanakwenda kujidhatiti ili wawe na timu imara zidi ya timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
“Tufanye mazoezi ili tupate stamina ambayo ni sehemu ya afya zetu napengine tukiunganisha na Watumishi wa wilaya zingine tunaweza kupata timu bora ya Watumishi Mkoa wa Singida,” amesema Kilala
Baada ya mchezo huo kukamilika Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba amesema kuwa wamedhihirisha umoja wao kwa kucheza michezo hiyo na kufanya kuwa Iramba na Mkalama kuwa ni moja huku akiahidi kuwa watakwenda Mkalama kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Godfrey Sanga ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa ukarimu waliowapatia.
MWISHO
Jemsi Tambue akiwa hewani kuwania mpira wa wavu katika mchezo uliowakutanisha timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Picha na Hemedi Munga
Kikosi cha timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakipanga kikiosi kitakacho anza zidi ya timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Kikosi cha timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kikiwa tayari kwa mtanange zidi ya timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Vikosi vyote viwili vikiwa tayari kwa mtanange wa ujirani mwema kati ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, B’hango Lyangwa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Godfrey Sanga akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni. Picha Hemedi Munga
Vikosi vyote viwili vikisikiliza nasaha baada ya dakika 90 kukamilika katika uwanja wa mabatini mjini kiomboi. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.