TIMU YA WATAALAMU KUTOKA OFISI YA RAIS UTUMISHI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA
Timu ya wataalamu kutoka @ofisi_ya_rais_utumishi imeendesha mafunzo ya tathmini ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma kupitia mfumo wa kielektroniki wa e-Utendaji.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 17 Juni 2025 katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Lengo la mafunzo hayo likiwa ni kuwajengea uwezo watumishi kuhusu namna ya kutumia mfumo wa e-Utendaji kwa ajili ya kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kitaifa.
Mfumo huu unatarajiwa kusaidia kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.