Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka Watumishi na Wananchi wa Wilaya ya Iramba kuitumia siku ya Jumamosi ya Kila juma kushiriki kwa ajili ya kufanya Michezo ya aina mbalimbali ili kuimarisha Afya zao dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Mwenda ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Jumamosi Novemba 16,2024 kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kiomboi Hospitali na kuhudhuriwa na Watumishi na Wananchi mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.
"Tumekuwa na majukumu mengi ya Ujenzi wa Taifa tumesahau kufanya Mazoezi kwa ajili ya kuimarisha Afya zetu dhidi ya magonjwa mbalimbali,kuanzia Sasa tutakuwa tunaitumia siku ya Jumamosi kufanya Michezo ya aina mbalimbali na ninatoa vifaa vya Michezo kama Jezi,Viatu,Mipira na vifaa vingine vya Michezo ya aina mbalimbali kwa lengo la kuongeza hamasa kwa Watumishi na Wananchi kufanya Michezo ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza" Amesisitiza DC Mwenda
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Daniel Paul Amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya kwa kutumia Wataalamu wa Afya wameweza kutoa Elimu kwa Watumishi na Wananchi kwenye maeneo mbalimbali Wilayani Iramba kuzingatia ulaji wa vyakula nyenye virutubisho Vyote,kufanya Mazoezi.
"Tumefanikiwa kutoa Elimu ya Afya na mtindo wa maisha huduma ya vipimo na ushauri na namna Bora ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza,kufanya Mazoezi kwa kutembea ila siku kilometa 2, Kufanya Mazoezi mepesi kupitia Muziki Maalumu wa Mazoezi ( Aerobick dance), Watumishi na Wananchi mbalimbali walishiriki kuchangia damu ili kiokoa maisha ya Watanzania mbalimbali yanayopotea kwa ajali na wakati wa kujifungua ambapo hukosa damu" Amesema Kaimu Mganga Mkuu
Maadhimisho ya Wiki ya Kuzuia magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika kuanzia Novemba 9, na kuhitimishaa Novemba 16,2024. Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Mwaka huu ni "MUDA NI SASA ZUIA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA MAHALA PA KAZI".
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.