UANZISHWAJI WA MADAWATI YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO NDANI NA NJE YA SHULE NI MUHIMU KATIKA KUMLINDA MTOTO- Dkt. BAGANDA.
Afisa Elimu Mkoa wa Singida Dkt. Elipidius Baganda amesema Serikali inaendelea kuhakikisha Ulinzi na usalama wa Mtoto unazingatiwa ili kutokomeza ukatili wa aina zote kwa Watoto waliopo ndani na Nje ya Shule.
Dkt. Baganda ameyasema hayo wakati akizungumza na Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa mtoto yanayotolewa na Programu ya Mradi wa Shule Bora kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ,Tarehe 31/03/2023 .
“Uanzishwaji wa Dawati hili Shuleni utasaidia kukabiliana na Ukatili unaojitokeza ndani na nje ya shule kwa wanafunzi na hata kwa watoto waliopo nyumbani na mitaani kwenu na nataka mfahamu kwamba kuna ukatili wa aina tatu kwa watoto ambao wa kwanza ni ukatili wa Kudhuru mwili, Wa pili ni ukatili wa Kingono na Wa tatu ukiwa ni ukatili wa Kihisia”.alisema Dkt. Bagenda.
Dkt Baganda aliendelea kwa kusema kwamba, Serikali inazidi kupambana na wimbi la ukatili linalo sababisha watoto wengi kukatisha ndoto zao, hivyo kuwasihi wanafunzi hao kuhakikisha wanapinga vikali ukatili wakianza na kutokufanyiana ukatili wao kwa wao.
“Kumekua na wimbi kubwa la Ushoga na usagaji ambalo chanzo chake kimebainika kuwa ni ukatili wa kingono wanaofanyiwa Watoto na kusababisha kuwapotezea dira kwenye Maisha yao”alifafanua Dkt. Baganda
Naye Mratibu wa Programu ya Mradi wa Shule Bora Mkoa wa Singida Ndugu Samwel Daniel ,Alimweleza Mgeni rasmi kuwa Programu hiyo inatekeleza maeneo manne ambayo ni ufundishaji,Ujifunzaji,Ujumuishi (Shule salama,watoto wenye ulemavu na Elimu kwa Msichana)na Uimarishaji wa mifumo. Mtoto kuwa salama shuleni inarahisisha Ujifunzaji wake.Pia Programu hii ya Shule Bora inatekelezwa kwenye Mikoa inayofanya vibaya Kitaaluma na moja ya sababu ni Usalama wa mtoto.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida bwana Edward Masero amewaambia washiriki wa mafunzo hayo Kuhakikisha wanatumia Miongozo iliyotolewa kwa ajili ya Kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa mtoto unawashirikisha Walezi,Wazazi na walimu wa Malezi waliopo shuleni.
“Mtu mwenye Uadilifu ni mtu ambaye anaweza kutunza siri utakapomwambia shida yako, Mtu anaefanya vizuri katika masomo yake ambae anaweza kubeba jukumu la ziada,Hivyo mnatakiwa kuhakikisha mnawasaidia watoto kuzitatua changamoto zao pindi wanapokuletea shuleni ”Alisema Masero.
Madawati ya ulinzi na usalama wa watoto 1,363 na Mabaraza ya watoto 562 katika mikoa 8 yameanziahwa tangu kampeni hii kuzinduliwa mwezi Juni, 2023.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.