By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga amewakumbusha wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa serikali ya vijiji na wajumbe wa kamati ya mitaa kuwa mwisho wa uwongozi wao ni Oktoba 22, 2019.
Hayo yameelezwa leo Jumatano Oktoba 23, 2019 katika mtandao wa kijamii wa Ofisi ya Rais Tamisemi wa Instagram.
Mapema leo Mhandisi Nyamhanga aliandika kwenye ukurasa wa Instagram kuwakumbusha viongozi hao.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha Mwenyekiti wa kijiji, Mwenyekiti wa kitongoji, Mwenyekiti wa mtaa, Wajumbe wa serikali ya kijiji na Wajumbe wa kamati ya mtaa kwamba ukomo wa uwongozi wao ni tarehe 22, Oktoba 2019.” Amesema Nyamhanga
Hayo yanakuja ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza mikoa yote na Halmashauri zote zilzofanya vizuri katika uandikishaji ambapo wote walipata asilimia 65 kwenda juu.
Huku Mkoa wa Singida ukishika nafasi ya 5 kwenye zowezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Wananchi wameombwa kujitokeza kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi kwa kuwa maendeleo yanaanzia huko kwa kupata viongozi wazuri huku wakiaswa kujiepusha na vitendo vya rushwa na kutakiwa kudumisha amani ambayo ndio tunu ya Taifa la Tanzania.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.