Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amekabidhiwa madawati 60 kutoka kwa Ushirika wa wachimbaji madini wa kisonga shelui (UWAWAKISHE) kata ya Mgongo Wilaya ya Iramba kwa ajili ya shule ya sekondari Mgongo ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Makundi mengine yaliochangia madawati ni Kijiji cha Mgongo Madawati 16, Kijiji cha Mseko Madawati 16, Mhe: Diwani wa kata ya Mgongo Madawati 10, Ndg. Athuman Swalehe Madawati 10, Ndg. Waziri Hussein Madawati 10.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ukamilishaji wa miundo mbinu katika shule ya sekondari ya mgongo. Ndg David Stephan alisema shule ya sekondari mgongo ilikuwa na upungufu wa madawati 63 na viti 92 hadi sasa hivi, kata imefanikiwa kutengeneza madawati 122 na viti 138 vyenye thamani ya Shilingi 7,800,000 ambao nimichango ya wananchi na Wadau mbalimbali.
Ndg. David Stephan aliongeza kusema, Wadau wengine wamechangia saruji mifuko 53 yenye thamani ya Shilingi 912,000 kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule ya sekondari ya Mgongo.
WACHANGIAJI WA SARUJI
|
IDADI YA MIFUKO
|
THAMANI
|
KANISA LA E.A.G.T MGONGO
|
5
|
85,000
|
KANISA LA K.K.K.T MGONGO
|
5
|
85,000
|
KANISA LA ANGLIKANA
|
1
|
17,000
|
MGODI WA MBUYUNI
|
17
|
300,000
|
UWAWAKISHE
|
20
|
340,000
|
KANISA LA F.P.C.T MGONGO
|
5
|
85,000
|
TOTAL
|
53
|
912,000
|
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo, Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula ameshukuru sana Ushirika wa wachimbaji madini wa kisonga shelui (UWAWAKISHE) na Wadau wa maendeleo wa kata ya Mgongo kwa ushirikiano mkubwa wa kutoa michango mbalimbali. “Tunawashukuru kwa kuwa mpo karibu nasi, tunawapenda sana kwa kuwa tunapowahitaji mnakaribia na mkishirikishwa katika maendeleo mbalimbali, ninawahakikishia madawati haya muliyoyatoa yatatumika vizuri na ufaulu wa watoto wetu utaongezeka zaidi.” Alisema Mhe: Luhahula
Mhe. Luhahula ametoa shukrani za dhati kwa wafadhili kwa uzalendo wao wa kutoa msaada kwa kuchangia mifuko ya saruji 53 yenye thamani za Kitanzania Shilingi 912,000 kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule ya sekondari ya Mgongo. Vile vile ameshukuru sana Ushirika wa wachimbaji madini wa kisonga shelui (UWAWAKISHE) kuhaidi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari mgongo ambayo itakabidhiwa Tarehe 28.02.2019.
Mhe: Luhahula ametoa wito kwa wananchi na wazawa wa Iramba waliopo ndani na nje ya Iramba kuiga mfano wa Ushirika wa wachimbaji madini wa kisonga shelui (UWAWAKISHE) na Wadau wa maendeleo wa kata ya Mgongo”. Malengo ya wilaya yetu ni kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma kwenye mazingira mazuri, ushirikiano wenu unahitajika sana kati ya serikali na Wadau wa maendeleo ili kuunga mkono jitihada za serikali” alisema Mhe: Luhahula.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.