Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Innocent Msengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wiki ya Chanjo akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda.
Hafla hiyo fupi ya uzinduzi imefanyika April 28, 2024 katika Zahanati ya Kiomboi na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Jeremia Kahurananga, Diwani wa Kata ya Kiomboi Omary Hassan, Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Zahanati na Wataalamu kutoka idara ya Afya na Wananchi mbalimbali.
Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo yameanza April 24, 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa April 30, 2025. Maadhimisho hayo yanaongozwa na Kauli Mbiu ya wiki ya Chanjo kwa Mwaka 2025 isemayo "TUUNGANE KUWEZESHA WALENGWA WOTE WAPATE CHANJO."

KIOMBOI, IRAMBA
Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Telephone: 026 - 2532253
Mobile: 026 - 2533001
Email: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.