Wapili kulia ni Afisa Tawala, Dijovison Ntangenki akiwahutubia maafisa mbalimbali katika siku ya Wiki ya Maji eneo la Maguli leo tarehe 18.03.2019. Mpiga picha Hemedi Munga
Afisa Tawala Wilaya ya Iramba, Dijovison Ntangeki, akiongea katika uzinduzi wa Wiki ya Maji leo tarehe 18/03/2019 katika vyanzo vya maji vya Mamlaka ya Maji, Mji wa Kiomboi eneo la Magula amewataka watu wa mamlaka ya maji kubadilika.
“ili kutunza miti inayopandwa na ingependeza sana kama tungepewa takwimu za mwaka jana miti mingapi iliyopanndwa na miti mingapi iloyokua.
Ninaagiza kwa Mamlaka ya Maji, miti tunayoipanda leo, miti mia moja angalau mwakani tukute 95% imekua, na jukumu la kuitunza miti hii ni la Mamlaka ya Maji na tusiache miti ijiotee, mifugo kuchungia, ngombe, mbuzi au wapita njia waingoe.”
Amemtaka Kaimu Mhandisi wa Maji Mhandisi Athumani Mkalimoto atakapokua anawaalika mwakani awe ni Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala au Afisa Tawala aje na taarifa ya maendeleo ya miti tunayoipanda leo na hii itutakua tunatekeleza kauli mbiu inayosema:
“Hakuna atakae achwa: Kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wote katika Dunia inayobadilika kitabia ya Nchi”
Naye Kaimu Mhandisi wa Maji Wilayani Iramba, Mhandisi Athumani Mkalimoto amesema” Kupitia Wizara ya Maji, tunaazimisha Wiki ya Maji na katika Wiki ya Maji tumesisitizwa kupanda miti kwenye vyanzo vya maji, kuelimisha jamii sheria ya maji ya mwaka 2019 sheria namaba 11 na kufundisha jumuiya.
Katika Dunia iliyobadilika kitabia ya Nchi, tunapanda miti ili kuhakikisha tunatunza vyanzo vyetu na tunakua na vyanzo endelevu vitakavyosababisha Mji wa Kiomboi unapata maji safi na salama kwa hali endelevu.
Akiongea katika uzinduzi huo, Fundi Sanifu, Juma Hamisi Makala amesema, tunapanda miti ili kuzuia vyanzo vya maji visiathirike na mabadiliko ya tabia ya Nchi na kutunza mazingira.
Naye Fundi sanifu, Naomi Elias Mkoma amesema, uzinduzi huu tunapanda miti mia moja katika kisima namba moja, namba mbili na namba tatu ili kulinda vyanzo vya maji eneo la visima na kuweka mazingira vizuri.
Afisa Tawala, Dijovison Ntangeki akipanda mti eneo la Magula leo tarehe 18.032019 katika Wiki ya Maji. Mpiga picha Hemedi Munga.
Kaim Mhandisi wa Maji Wilayani Iramba, Mhandisi Athumani Mkalimoto akipanda mti eneo la Magula leo tarehe 18.03.2019 katika Wiki ya Maji. Mpiga picha Hemedi Munga
Kaim Mweka Hazina Wilayani Iramba, Prosper Banzi, akipanda mti eneo la Magula katika Wiki ya Maji leo tarehe 18.03.2019. Mpiga picha Hemedi Munga.
Afisa TEHAMA Wilayani Iramba, Hemedi Munga akipanda mti eneo la Magula leo tarehe 18.03.2019 katika Wiki ya Maji. Mpiga Picha Prosper Banzi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.