VIONGOZI IRAMBA WAPONGEZWA KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndugu Ismail Ali Ussi, amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Ndugu Michael Agustino Matomora, pamoja na Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa usimamizi bora wa miradi ya maendeleo na ushirikiano mzuri baina yao na viongozi wengine Wilayani hapo.
Pongezi hizo zilitolewa Julai 21, 2025, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Nsunsu katika Kata ya Ntwike, mradi wenye thamani ya Shilingi milioni 415.7 unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya wakazi 4,299 wa Kijiji cha Nsunsu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.