Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Iramba Mwl.Linno Mwageni amekabidhiwa madawati 25 yenye thamani ya shilingi 2,750,000 kutoka kwa Wadau wa maendeleo ya Ruruma (Ruruma development club-RDC) kwa ajili ya shule ya msingi Ruruma ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo, Mwl. Mwageni ameshukuru sana Wadau wa maendeleo ya Ruruma kwa ushirikiano mkubwa wa kutoa michango mbalimbali. “Tunawashukuru kwa kuwa mpo karibu nasi, tunawapenda sana kwa kuwa tunapowahitaji mnakaribia na mkishirikishwa katika maendeleo mbalimbali, ninawahakikishia madawati haya muliyoyatoa yatatumika vizuri na utaona ufaulu wa watoto wetu utaongezeka zaidi.” Alisema Mwl. Mwageni.
Aidha ametoa shukrani za dhati kwa mfadhili mzawa Bwana. Joseph Katala kwa uzalendo wake wa kutoa msaada wa madawati 40 yenye thamani ya Shilingi za kitanzani milioni 3 na kusaidia ukarabati wa vyumba 2 vya madarasa. Vile vile amemshukuru mwandisi Jumbe Katala kwa kuchangia mifuko 24 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa chumba cha darasa.
Mwl. Mwageni ametoa wito kwa wananchi na wazawa wa Iramba waliopo ndani na nje ya Iramba kuiga mfano wa wanajumuiya ya maendeleo wa Ruruma (Ruruma development club-RDC).” Malengo ya Halmashauri ni kuandikisha wanafunzi 8227 kwa darasa la kwanza wakiwemo wavulana 4221 na wasichana 4006, kwa idadi hii lazima mahitaji ya samani, walimu na miundombinu yataongezeka. Yote haya ni ya msingi hivyo ushirikiano wenu unahitajika sana kati ya serikali na Wadau wa maendeleo ili kuunga mkono jitihada za serikali” alisema Mwl. Mwageni.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akiwa katika picha ya pamoja na wanajumuiya wa maendeleo ya Ruruma wilayani Iramba mkoa wa Singida.
Wanajumuiya wa maendeleo ya Ruruma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni katika hafla ya kukabidhiana madawati katika shule ya msingi Ruruma kata ya Kiomboi wilayani Iramba mkoa wa Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.